Tuesday, 3 September 2019

WAZIRI KALEMANI AWASHA UMEME VIJIJI VYA NJOMBE

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani(kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Lupembe,Joram Hongoli (kushoto) wakipitia orodha ya vijiji vilivyopata na visivyopata katika jimbo hilo ili vile ambavyo bado viweze kupatiwa umeme.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wanakijiji wa Lole kabla ya kuwasha umeme katika kijiji hicho katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, mkoani Njombe

Baadhi wa wanakijiji wa Lole, katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, mkoani Njombe, wakimshuhudia, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani( haonekani pichani) akiwasha umeme katika moja ya nyumba za ibada katika kijiji hicho.

Wanakijiji wa Kijiji cha Ninga, katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, mkoani Njombe,wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kuhusu mradi wa usambazaji wa umeme vijiji (REA), kabla ya kuwasha umeme katika kijiji hicho.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( kulia) akitoa maelekezo ya kuboresha na kuharakisha utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijiji ( REA) kwa wakandarasi wanaotekeleza mradi huo wa Kampuni ya JV Mufindi Power Service Ltd na Hegy Engineering Service Ltd, Shirika na Umeme nchini (Tanesco), na Wakala wa Nishati vijijini REA.

No comments:

Post a Comment