Wednesday, 4 September 2019

UBA TANZANIA YALENGA KUPUNGUZA TATIZO LA VITABU KWA KUGAWA VITABU VYA FASIHI SHULE ZA SEKONDARI TABATA DAR ES SALAAM

  UBA Tanzania wakikabidhi vitabu vya fasihi kwa mkuu wa shule ya sekondari Ugombolwa Simon Machia pamoja na Afisa Mtendaji kata Eligius Mulokozi na wanafunzi wa shule hiyo siku benki ya UBA ilipotembelea kwaajili ya kugawa vitabu hivyo
Asupya Nalingigwa, mkuu wa kitengo cha Digital Banking akikabidhi vitabu kwa wanafunzi wa shule ya Migombani sekondari siku benki ya UBA Tanzania ilipotembelea shule hizo zilizopo Tabata Jijini Dar es salaam

 Mkuu wa kitengo cha Digital Banking kutoka UBA Tanzania, alikimkabidhi vitabu makamu mkuu wa shule ya sekondari ya Zawadi, Dativa Ngowi, siku walipotembelea shule za sekondari Tabata na kugawa vitabu vya Fasihi


Mkuu wa kitengo cha Digital Banking, Asupya Nalingiwa akitoa mawaidha kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ugombolwa, juu ya umuhimu wa usomaji vitabu siku UBA Tanzania walipotembelea  shule za Tabata jijini Dar es Salaam na kugawa vitabu vya Fasihi
                                                        xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

 UBA Tanzania, siku ya Ijumaa ilitembelea shule mbalimbali za Sekondari za serikali zilizopo Tabata jijini Dar es salaam nakugawa vitabu vya fasihi simulizi kama moja ya njia za kupunguza tatizo la upungufu wa vitabu kwenye shule mbalimbali za Tanzania hasa za serikali.

Shule ambazo zimeangukiwa na neema hiyo ni pamoja na shule ya sekondari ya ugombolwa,Miombani na shule ya sekondari ya Zawadi. Vitabu mbalimbali viligawiwa vikiwemo Things fall apart, The fishermen, The girl that can pamoja na Fine Boy kutoka kwa waandishi maarufu kamavile Chinua Achebe na Chigozie Obioma.


UBA Tanzania imekua mstari wa mbele katika kusaidia ukuaji wa elimu Tanzania kwa kugawa vitabu kwenye shule za sekondari pamoja na kuwezesha miundombinu mbalimbali katika sekta ya elimu.


Akiongea na wanafunzi hao, Asupya Nalingigwa mkuu wa kitengo cha digitali, aliwaambia wanafunzi faida za usomaji vitabu badala ya kujikita zaidi na mambo yasiyo ya muhimu kwenye mitandano ya kijamii.


 Aidha amewashauri wanafunzi kutumia mitandao hiyo kwa kujisomea Zaidi na kujifunza mambo yenye tija.

Mkuu wa shule ya Ugombolwa  Simon Machia ameshukuru msaada uliotolewa na UBA Tanzania na kuwasihi wanafunzi kutumia vitabu hivyo kwa makini na kuongeza ufahamu ili benki ione faida iliyotokana na kupokea vitabu hivyo.


Uongozi wa shule za Miombani na Zawadi pia wamefurahishwa na ugawaji wa vitabu hivyo na kusema kuwa benki haikua na upendeleo na imewaona hata wao ambao shule zao bado zinajikokota ili kufikia malengo na kupanda ngazi kimkoa au kitaifa.


Mbali na uhitaji wa vitabu walimu wakuu hao wameeleza kuwa kuna mahitaji mengine mbalimbali kama vile upungufu wa madarasa ya kusomea, Viti, Meza, Madawati, Komputa pamoja na uzio wa shule ili kuboresha usalama.

No comments:

Post a Comment