Tuesday, 3 September 2019

Spika wa Bunge, Job Ndugai Amwapisha Miraji Mtaturu Kuwa Mrithi wa Jimbo la Tundu Lissu

Spika wa Bunge, Job Ndugai, leo Jumanne September 3, 2019  amemwapisha Miraji Mtaturu kuwa Mbunge wa Singida Mashariki. Mtaturu amechukua nafasi iliyoachwa na Tundu Lissu.

Wakati Mtaturu akiapishwa, wabunge wa CHADEMA wamesusia tukio hilo kwa kugoma kuingia ukumbini .

Wakati Mtaturu akichukua nafasi yake, Ndugai amesema jimbo hilo sasa limepata mwakilishi halali.

No comments:

Post a comment