Monday, 2 September 2019

Rais Shein afanya uteuzi huu


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amemteuwa Dkt. Zakia Mohammed Abubakar kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

Dkt. Zakia anachukuwa nafasi iliyowachwa wazi na Profesa Idris Ahmada Rai ambae anamaliza muda wake wa kutumikia wadhifa huo kwa mujibu wa sheria.

Uteuzi wa Dkt Zakia umefanyika kwa mujibu wa uwezo aliopewa Rais, chini ya kifungu cha 9 (1) cha Sheria ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, namba 8 ya mwaka 1999.

Aidha, uteuzi huo utaanzia Septemba, 06, mwaka huu.

No comments:

Post a comment