Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Vijana walioshiriki katika mafunzo ya ukuzaji ujuzi kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba (Green House) katika Kijiji cha Ihemi alipotembelea eneo hilo kukagua maendeleo ya mafunzo hayo Mkoani Iringa.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa Bi. Lucy Nyalu akieleza jambo kuhusu ushirikishwaji wa vijana kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa huo walioshiriki katika mafunzo hayo.

Baadhi ya Vijana wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea vijana hao kwa lengo la kukagua maendeleo ya mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya kitalu nyumba.
Mratibu wa Mradi huo katika Halmashauri ya Iringa Vijijini Bw. Daniel Mlay akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ukuzaji ujuzi kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipewa maelezo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Holly Green Bw. Octavian Laswai alipokuwa akikagua kitalu nyumba wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mafunzo ya kilimo cha kisasa kupitia kitalu nyumba, Mkoani Iringa.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ihemi Bw. Antony Akata (wa pili kutoka kushoto) akimfafanulia jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea eneo hiyo kwa lengo la kukagua maendeleo ya mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya kitalu nyumba.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mafinga Bi. Saada Mwaruka alipokuwa akikagua chanzo cha maji yanayotumika kumwagilia Kitalu nyumba hicho. (Katikati) ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Venerose Mtenga.

******************

Programu ya ukuzaji ujuzi kwa vijana kupitia teknolojia ya Kitalu nyumba (Green house) inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imewapa hamasa vijana kushiriki kwa wingi kwenye sekta ya kilimo ikiwa ni chanzo cha kimoja wapo cha ajira nchini.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati wa Ziara yake ya kukagua maendeleo ya mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba, Mkoani Iringa.

Waziri Mhagama alieleza kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu iliamua kuanzisha programu hiyo kwa lengo la kuwawezesha vijana kushiriki kwa wingi kwenye masuala ya kilimo ili waweze kujiajiri wao wenyewe na kuajiri vijana wenzao kupitia teknolojia hiyo.

“Mradi huu unatekelezwa kwenye Halmashauri 185 nchini katika awamu hii ya kwanza ikiwa na lengo la kuwawezesha vijana kuwa na ujuzi pamoja na stadi za kilimo cha kisasa kupitia kitalu nyumba ambacho kina tija katika kuwapatia mazao bora na mengi yatokanayo kwenye eneo dogo,” alieleza Mhagama

Alieleza kuwa Serikali imeendelea kuwawezesha na kuwajengea uwezo vijana wa masuala ya ukuzaji ujuzi ili waweze kuongeza tija kwenye shughuli wanazozifanya na zitakazo wakwamua kiuchumi.

“Vijana wanaweza kupata ajira bora katika kilimo endapo watawekewa mazingira bora kama kuimarisha teknolojia na mbinu za kilimo,” alisema Mhagama.

Hata hivyo aliwasihii vijana kuhakikisha wanatunza vitalu nyumba hivyo kwa kuwa watanufaika navyo na vitawasaidia kufanilisha malengo yao sambamba na kuleta maendeleo endelevu katika sekta ya kilimo.

Aidha alitoa wito kwa wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuhakiksha wanawasilisha njia bora zaidi za kuwapata vijana stadi zitakazo wajengea uwezo kupata teknolojia za kisasa zitumikazo katika kilimo pamoja na kuwapatia mitaji ambayo itawawezesha kujenga vitalu nyumba vyao binafsi.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Venerose Mtenga alisema kuwa Ofisi hiyo inatekeleza programu mbalimbali zitakazo wawezesha vijana kupata ujuzi na stadi stahiki zitakazo wasaidia kuondokana na changamoto ya ajira.

Naye Mratibu wa Mradi huo katika Halmashauri ya Iringa Vijijini Bw. Daniel Mlay alisema kuwa jumla ya vitalu nyumba vinne vimejengwa na vijana 431 wameweza kunufaika na mafunzo hayo.

“Tutaendelea kuwahamasisha vijana washiriki kwa kikamilifu katika mradi huu kwa kuwa una manufaa mazuri kwao,” alisema Mlay 

Pia mmoja wa vijana walionufaika kupitia Mradi huo Bw. Ramadhani Haule alieleza kuwa mradi huo wa Kitalu Nyumba umewasaidia kupata elimu bora ya kilimo na umesaidia vijana kuondoka kwenye makundi ya wasiokua na ajira.

“Tunaishukuru Serikali kwa kutuamini na kutupatia ujuzi huu, tunaahidi tutaendelea kushirikiana vijana wengi ili kujikwamua kiuchumi,” alisema

Katika ziara hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alitembelea Vitalu Nyumba vilivyopo katika eneo la Ihemi na Halmashauri ya Mafinga.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: