Tuesday, 3 September 2019

Pacha aliyetenganishwa na mwenzake baada ya kuzaliwa wakiwa wameungana afariki Dunia

Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Muhimbili Dkt.Suphian Baruani amesema Mtoto Anisia, pacha aliyetenganishwa na mwenzake baada ya kuzaliwa wakiwa wameungana amefariki Dunia Muhimbili  siku chache tangu waliporejea Nchini kutoka Saudi Arabia walikofanyiwa upasuaji.

Akizungumzia chanzo cha kifo cha mtoto huyo daktari bingwa wa upasuaji wa watoto,  Petronilla Ngilino amesema wakati wanaendelea kumfanyia uchunguzi alianza kutapika.

Amesema walipomuuliza mama yake  alisema alianza kutapika tangu wakiwa kwenye ndege na akawa ameishiwa nguvu.

“Tulianza kumuwekea maji kwa kuwa yalikuwa yanapungua, na tukazuia matapishi yasiingie kwenye mfumo wa hewa. Tuliendelea na uchunguzi tukabaini kuna tatizo kwenye tumbo lake,” amesema Dk Ngilino.

Amesema utumbo wa mtoto huyo ulikuwa umejifunga ndipo walipofikia uamuzi wa kumfanyia upasuaji kurekebisha hilo ambapo hata hivyo mtoto huyo alifariki Dunia

No comments:

Post a comment