Friday, 6 September 2019

KAMPUNI YA BIA TANZANIA (TBL) YAENDELEA KUFANYA VIZURI KIBIASHARA

Licha ya changamoto za kibishara zilizokuwepo katika kipindi cha mwaka uliopita, kampuni ya Bia Tanzania (TBL) chini ya kampuni ya kimataifa ya ABInBEV, imeendelea kufanya vizuri kibiashara na kuchangia pato la serikali kupitia kodi sambamba na kutekeleza miradi mbalimbali ya kusaidia jamii. Hayo yamebainishwa katika mkutano Mkuu wa 46 wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam,ambapo imeelezwa kuwa faida ya kampuni hiyo imeongezeka kwa asilimia 15 na kuwezesha wanahisa wake kupata gawio la shilingi 350 kwa kila hisa.
Mwenyekiti wa Bodi ya TBL, Mh. Cleopa Msuya,(katikati) akifafanua jambo katika mkutano wa wanahisa,wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa TBL,Philip Redman (kulia)na Katibu wa bodi,Huruma Ntahena.
Baadhi ya wanahisa wakifuatilia ajenda za mkutano na kushiriki kutoa mapendekezo
Mwenyekiti wa Bodi ya TBL, Cleopa Msuya na Mkurugenzi wa TBL, Philip Redman wakiongea na waandishi wa habari.

No comments:

Post a Comment