Thursday, 5 September 2019

HALMASHAURI JIJI LA ARUSHA,WADAU WAENDELEZA KAMPENI YA TALII KASKAZINI

Halmashauri ya jiji la Arusha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya utalii imeendelea kuendeleza kampeni ya Talii Kaskazini kwa kushirikisha wanafunzi wa shule ya msingi ya Arusha School kwa kutembelea makumbusho ya elimu ya viumbe na makao makuu ya jiji la Arusha.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa mkakati wa kutangaza utalii wa ndani Kanda ya Kaskazini kwa lengo la kuhamasisha utalii wa ndani kwa kujumuisha Mikoa ya Kilimanjaro,Arusha,Tanga na Manyara ambapo wanafunzi hao wamepata fursa ya kujifusa historia ya jiji la Arusha.

Afisa Utalii jiji la Arusha Michael Ndaisaba amesema kuwa kampeni hiyo ambayo imeanza katika jiji la Arusha kwa kuhamasisha wanafunzi licha ya kuwa ni sehemu yao ya mafunzo ni wadau wakubwa wa utalii wa ndani katika jamii.

Ndaisaba ameongeza kuwa kampeni hiyo pia imelenga kukuza mahusiano ya taasisi zinazohusika na utalii na zitakazoshiriki kutekeleza mkakati wa vivutio vya utalii kwa wakazi wa Kanda ya Kaskazini ili kuweza kuwekeza kwenye utalii kwa gharama nafuu na rahisi kufikika.

Sambama na hayo ameeleza melengo mengine ya kampeni hiyo ni kukuza utamaduni kwa vijana kupenda kutalii na hatimaye kuongeza idadi ya watalii wa ndani ifikapo mwaka 2021.

Vilevile amesema kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya utalii nchini wakiwemo Tanzania Tourist Board(TTB),TANAPA na TAWA walengwa wa mkakati huo ni wakazi wa Kaskazini mwa Tanzania wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi,sekondari na vyuo bila kuwasahau wananchi wa kawaida,taasisi za fedha,vikundi mbalimbali vya kijamii pamoja na wafanyabiashara ambapo kauli mbiu katika kampeni hiyo ni UTALII WA NDANI UNAANZA NA WEWE,TWENDE TUKATALII.
 Wanafunzi wa shule ya msingi ya Arusha School walipotembelea Makumbusho ya elimu ya viumbe jijini Arusha katika kuendeleza kampeni ya Talii Kaskazini
Wanafunzi wa shule ya msingi Arusha School wakiwa nje ya jengo la Makao Makuu ya jiji la Arusha wakipewa maelekezo katika kampeni ya Talii Kaskazini

No comments:

Post a Comment