Monday, 19 August 2019

UVCCM Tabora Mjini Wachangia Damu Waathirika Wa Ajali Ya Moto Morogoro


 Pichani  ni benki za damu zilizotolewa na vijana wa UVCCM Tabora mjini.
Pichani ni mmoja wa  vijana wa UVCCM Tabora akitoa Damu kwa ajili ya ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro.

 Pichani ni vijana wa UVCCM  Tabora mjini wakiwa na tayari wametoa  Damu.

Umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Tabora mjini(UVCCM) wamejitokeza na kuungana na baadhi ya watanzania kuendelea kuchangia Damu kwa ajili ya majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea huko mkoani Morogoro 

Taasisi hii ni ya pili kwa mkoa wa Tabora kujitokeza kuchangia Damu kwa ajili ya majeruhi wa ajali hiyo ya moto, ambapo hapo awali chama cha bodaboda na bajaji mkoa wa Tabora ndicho kilichoanza kufanya zoezi hilo ambalo tayari waliweza kukabidhi chupa za Damu miamoja katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Kwa upande wa Mwenyekiti wa UVCCM Tabora mjini Ibrahimu Songoro amesema wameguswa na tukio hilo la ajali ya moto hivyo Wamefanya uamuzi wa kujitolea Damu kwa watanzania wenzao waliofikwa na tukio hilo

"Watanzania ni wamoja na sisi vijana wa chama cha Mapinduzi ni wamoja pia tunatakiwa kujali Maisha ya mtu na kujali uthamani wa utu wa vijana wetu nchi nzima kwa hiyo vijana waliopata matatizo na janga la moto mkoani Morogoro tunajiona ni kama sisi matatizo hayo ni ya kwetu na ndio maana leo tumechukua jukumu letu lakuchangia Damu kwa hiari Ili kuweza kusaidia maisha ya wenzetu wanaohangaika kwa kukosa Damu"Amesema Songoro.

No comments:

Post a Comment