Muwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Marlin Komba,akizungumza na mabalozi katika mkutano mkuu uliofanyika Jijini Mwanza leo.30/8/2019.Picha zote na habari zimeandaliwa na Vero Ignatus .
John Seka Afisa mtendaji mkuu wa Taasisi ya Mabalozi wa Usalama barabarani Nchini.(RSA )akizungumza na mabalozi katika mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika Jijini Mwanza.
 Naadhi ya mabalozi wa Usalama barabarani wakiwa katika picha ya pamoja kuelekea katika mkutano mkuu wa mwaka Jijini Mwanza leo 30/8/2019
 Mabalozi wa usalama barabarani wakionekana katika picha ya pamoja Jijini Mwanza leo tarehe 30/8/2019
Mwawakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Marlin Komba ,akisisitiza jambo katika mkutano mkuu wa mwaka wa mabalozi wa usalama barabarani uliofanyika Jijini Mwanza leo.30/8/2019

Mabalozi wa usalama barabarani nchini wakiwa katika mkutano mkuu wa Mwaka uliofanyika Jijini Mwanza leo 
 Moja ya timu wapenzi na madhafiki wa Simba sports Club wakiwa uwanjani kwaajili ya mchezo wa kirafiki katika Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
Moja ya timu wapenzi na madhafiki wa Yanga  sports Club wakiwa uwanjani kwaajili ya mchezo wa kirafiki katika Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.

Na .Vero Ignatus ,Mwanza

Zaidi ya mabalozi 125 kutoka Taasisi ya Mabalozi wa usalama barabarani( RSA )wamekutana  Jijini Mwanza,lengo kuu likiwa ni  kutoa Elimu na kuwajengea wananchi  uwezo wa  kuwa sehemu ya mabadiliko ya usalama barabarani ikiwa ni namna  ya kusaidia kupunguza ajali ,kwani kila raia wa Tanzania anawajibu wa kuwa sehemu ya mabadiliko ya usalama barabarani.

John Seka Afisa mtendaji mkuu wa Taasisi ya mabalozi wa usalama barabarani Nchini, amesema kwa kushirikiana na jeshi la Polisi Kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Mwanza kikisimamiwa na RTO,Tanroad ,Jeshi la zimamoto, walifanya zoezi za kurudishia alama za barabarani zile zilizopauka ,na kuchora mpya sehemu zinazohitajika.

Seka amesema kuwa kazi zao kubwa  kama RSA ni kukemea, kuelimisha ,kutoa taarifa pale dereva anapokwenda kinyume na taratibu na sheria za usalama barabarani ili kuhakikisha kuwa ajali zinapungua kama siyo kwisha kabisa

Sisi tunafanya kazi zetu kama polisi jamii,macho yetu tunayaelekeza kwa kutambua kuwa jeshi la polisi peke yao hawawezi kwani askari ni wachache na vitendea kazi ni vichache je! sisi kama wananchi hatuna wajibu wa kupunguza?aliuliza Seka.”

Augustus Fungo ni Mkurugenzi wa tafiti za kisheria kutoka RSA amesema kuwa pamoja na kuwa balozi lazima wazingatie sheria za usalama barabarani pia lazima wafuate sheria kama utaratibu unavyoagiza
Amesema hadi sasa RSA wanatekeleza mradi  wa Maboresho ya sheria ya  usalama barabarani,wenye lengo la kushawishi serikali na bunge kubadili sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1973  ili ikidhi mahitaji ya wakati huu kwasababu ina mapungufu katika maeneo mbalimbali.

’’Mfano wa mapungufu hayo ni pamoja na sheria ya sasa kutomlazimisha abiria kuvaa kofia ngumu,kufunga mkanda,kutokulazimu magari madogo kuwa na vizuizi vya watoto wakiwa ndani ya gari (child restraint) Sheria pia hailazimishi magari yote kusimama kabla ya kuvuka kivuko cha reli isipokuwa magari ya abiria na mizigo .Alisema Fungo’’

Amesema hadi sasa RSA imefanikiwa kufungua klabu za usalama barabarani kwa wanafunzi katika shule 22,ambapo 10 kutoka mkoa wa Kilimanjaro,12 mkoa wa Pwani, amesema matazamio ya baadae ni kupanua wigo wa shule zinazopata elimu ya usalama barabarani nchini Tanzania.

“Kwa kuwa tunaamini watoto wakifundishwa tangia wakiwa wadogo ni rahisi wao kuelewa zaidi kwao kutii sheria na kujiepusha na ajali”alisema Fungo

Akizungumza muwakilishi wa Katibu mkuu wizara ya mambo ya Ndani Marlin Komba amemtaka kila balozi kutimiza wajibu wake kwa kuzingatia maadili,bila kuwa na ushabiki wowote,pasipo kuwatetea wavunja sheria za usalama barabarani,badala yake watumie ubalozi wao kwenye kuelimika na kupata maarifa.

“Kama wewe mwenyewe huwezi kuwa na nidhamu mahali unapooneka je ukiwa peke yako utaionyesha ,nidhamu ni kusikiliza na kuelewa “alisema Marlin

Amewataka kwenda kuwa mabalozi kwa watu wengine ili kufanya maamuzi sahihi kuzingatia sheria na usalama barabarani ,nakuepuka lugha za matusi kwani ni kosa la jinai,huku akiwaonya baadhi ya mabalozi kutokutumia nembo ya RSA kukashifu watu wengine,amewataka kutumia utaratibu unaostahili

Siku hiyo ya mabalozi wa usalama barabarani imebeba kauli mbiu isemayo ,uchumi wa viwanda unahitaji kufanyika kwa mabadiliko ya sheria ya Usalama Barabarani,ili kulinda rasilimali watu dhidi ya ajali.  

Mkutano huo uliambatana na michezo mbalimbali ukiwemo mchezo wa mpira wa miguu,kuvuta kamba kufukuza kuku na mbio za magunia ,ambapo michezo yote ilifanyika katika uwanja wa mpira wa Nyamagana Jijini Mwanza.

MWISHO
















Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: