Jumuiya ya wazazi mkoa wa Morogoro imempongeza Mhe Rais wa  jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kufanya mkutano wa kihistoria na wafanyabiashara watano kutoka kila wilaya na kuchukua hatua za haraka za kufanya mabadiliko maeneo yenye madhaifu,

hayo yamesemwa leo hii na mwenyekitibwa jumuiya ya wazazi (CCM) mkoa wa Morogoro Komredi Francis Heri Hoza wakati akiongea na mamia ya waendesha bajaji wa mkoa wa Morogoro wakati wa kufungua mkutano wa uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya wa chama chao uliofanyikia ukumbi wa Rose Garden uliopo Mafiga Morogoro majira ya saa kumi jioni

Hoza ambaye aliambatana na katibu wa Uvccm wilaya ya Morogoro vijijini ndg Mussa Yusuph Alisema "" Kwa niaba ya jumuiya ya wazazi mkoa wa Morogoro tunapenda kwa dhati kumpongeza Mhe Rais kwa kufanya mkutano wa kihistoria na wafanyabiasha wa kutoka wilaya mbalimbali nchini na kupokea changamoto zao kisha kuchukua hatua kwa kufanya mabadiliko maeneo yenye madhaifu kwa maslahi ya taifa, ni jambo la kupongezwa sana" Hoza amesema mkutano ule umefungua mlango mpya katika sekta ya biashara na uwekezaji nchini na anatumai kabisa maelekezo na nia ya Mhe Rais ikifuatwa kwa vitendo na watendaji, basi kasi ya ukuaji wa uchumi itakwenda kwa kasi sana katika awamu hii ya tano " Naamini kwa dhati kabisa ya kwamba mkutano ule baina ya wafanyabiashara na mhe Rais utafungua milango mipya ya ukuaji wa sekta ya biashara na uwekezaji nchini hivyo nitoe wito kwa watendaji kutekelekeza kwa vitendo nia na maelekezo ya mhe Rais ili kufikia adhima yetu ya kuwa taifa la viwanda"

Katika kusisitiza mwenyekiti wa wazazi mkoa wa Morogoro komredi Francis Heri Hoza amesema mhe Rais Dr John Pombe Magufuli mbali ya kufanya majikumu yake kama Rais lakini sasa pia amekuwa ni mwalimu wa watendaji, viongozi na vijana wa taifa la kesho wa namna viongozi na watendaji wa serikali wanapaswa kuwa, hususani katika kutimiza majulumu yao ipasavyo "Mhe Rais wa awamu ya tano anatufundisha kwa vitendo namna gani viongozi mbalimbali na watendaji wanapaswa kuwa katika kutimiza majukumu, mbali ya kuwa mhe Rais wetu, lakini atabaki kuwa kwenye kumbukumbu ya kudumu katika historia ya nchi na vizazi vya sasa na vijavyo kama mwalimu anayefundisha taifa namna ya kuwajibika ipasavyo"

Pia aliwataka waendesha vyombo vya usafiri pote nchini kuwa na vyama ambavyo mbali ya kushughulikia changamoto zao za kazini, lakini wataweza kupata mikopo na kubuni miradi mbadala itakayowawezesha kushiriki kikamilifu shuhuli za kiuchumi na kujikwamua kimaisha na kuchangia pato la taifa

Nae mwenyekiti wa chama hicho cha waendesha bajaji ambae amepita bila ya kupingwa Ndg Rajabu Juma Sikiweni amesema wataendelea kufanyakazi kwa bidii ili kuchangia uchumi wa nchi na kukishukuru chama cha mapinduzi mkoa wa Morogoro kwa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia utekelezaji wa ilani ikiwamo maswala mbalimbali ya wasafirishaji mkoani humo

Katika mkutano huo ndg Rajabu Juma Sikiweni alipita bila ya kupingwa nafasi ya uwenyekiti, ndugu Omari Mpulila katibu, Yohana Kisusi makamu mwenyekiti na Salumu Mnangwa mwekahazina

Na Fatima Mtengeta
Morogoro
Share To:

msumbanews

Post A Comment: