Watu Wenyeulemavu wametakiwa kuchangamkia fedha za mkopo bila riba walizotengewa na Serikali ambazo zipo katika Halmshauri ya miji nchini.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu, Stellah Ikupa wakati akihutubia kwenye Tamsha la Kitaifa la kupinga Unyanyasaji na Ukatili wa kijinsia kwa watu wenye ulemavu lililoandaliwa na Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO) lililofanyika Jijijini Dodoma wiki iliyopita.

“Changamukieni fedha hizo ambazo ni asilimia mbili zipo kwenye halmshauri zetu tena mnakopa bila ya kuwa riba yoyote waambieni na wenzenu” alisema Ikupa.

Alisema awali wanawake na vijana kila kundi lilitengewa asilimia 5 ya fedha kwa ajili ya kukopeshwa lakini baada ya waziri huyo na wenzake kuomba kusaidiwa walemavu kila kundi lilitoa asilimia moja na kuwa mbili kwa ajili ya watu wenye ulemavu.

Ikupa alisema Serikali imekuwa ikiwajali sana watu wenyeulemavu ndio maana imetenga wizara hiyo ambayo inashughulikia masuala yote yanayo wahusu walemavu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: