Sunday, 5 May 2019

WASAFIRISHAJI WANENA MAZITO JUU YA MAREHEMU MENGI.

“Ni Mzalendo, ni mtu muhimu aliyepigania usawa kwa maisha ya Watanzania wengi, ametutoka kipindi ambacho Taifa linamuhitaji zaidi.” Amesema Rais wa Chama Cha Wasafirishaji Tanzania TAT Mohammed Abdullah Es-Haq

“Amekuwa na mchango mkubwa katika sekta tofauti nchini, Daima mchango wake hautasahaulika, napenda kutoa pole kwa Familiya, Ndugu, jamaa na Wafanyakazi wa IPP kwa msiba huu mkubwa, Mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki kigumu” ameeleza Mohammed kwa majonzi mazito.

“MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI.”

No comments:

Post a comment