Sunday, 19 May 2019

Viongozi Wa Dini Arumeru Watakiwa Kuwaeleza Wananchi Ukweli

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,  Jerry Muro akizungumza katika kongamano la viongozi wa dini lililofanyika jana katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu, Patandi. ambapo alisemakuwa niwajibu wa kila mchungaji kuwaamasisha waumini wao kufanya kazi. 
Mtume Sekela Lolandi wa Huduma ya Ngurumo ya Upako akitoa neno katika Kongamano la Vingozi wa Dini, lililofanyika jana katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu, Patandi. 
baadhi ya viongozi wa dini wakiwa wanasikiliza kwa makini wakati mkuu wawilaya ya meru akiongea nao.


Na Woinde Shizza , Arusha

Viongozi wa dini wametakiwa kuwaeleza wananchi wao umuhimu wa kufanya kazi kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza tatizo la umaskini linalowakabili wananchi wengi. 

Hayo yalibainishwa jana na mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro wakati akizungumza katika kongamano la viongozi wa dini lililofanyika jana katika ukumbi wa chuo cha ualimu patandi ambapo alisemakuwa niwajibu wa kila mchungaji kuwaamasisha waumini wao kufanya kazi. 

Alisema kuwa kumekuwa na tabia ya wananchi wengi kulalamika hali ngumu ya kimaisha lakini ukiwachunguza zaidi unakuta hawana kazi yeyote wanaofanya zaidi ya kulalamika tu hali ngumu ya Maisha

"napenda kuwaomba viongozi wangu wadini mtusaidie hawa waumini wenu wakija uko kutaka kuwaombea wachunguzeni kwanza kama wanakazi kama hawana wahamasisheni wafanye kazi nasio wakae tu bure na kulalamika hali ngumu ya kimaisha "alisema Muro

Aidha Muro aliwasihi viongozi hao wa dini kuendelea kuombea amani ya nchi yetu, pamoja na kuombea viongozi wa nchi yetu. 

Wakati huo huo Watanzania wametakiwa kuendeleza kuenzi upendo, mshikamano, na amani tulioasisi na baba wa Taifa kwani amani hii ikipotea kuirudisha ni kazi na itatugarimu. 

Hayo yameelezwa na mtume Sekela Lolandi  wa Huduma ya ngurumo ya upako  iliopo ndani ya wilaya ya Arumeru,wakati akiongea Katika kongamano la wachungaji la kuombea wilaya ,mkoa ,Taifa na viongozi wa serikali  kongamano lililoandaliwa na mkuu  wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro ambapo walisema kuwa ni wajibu wa kila wananchi kuenzi amani tuliachia. 

Alisema kuwa  niwajibu wa kila mtanzania kuenzi amani na upendo pamoja na ushirika tulioasisiwa na wazee wetu kwani amani hii ikitoweka tutakuwa tumepoteza kitu kikubwa mno ambacho itakuwa ni ngumu kuirejesha. 

"watanzania tunatakiwa tuwe na umoja upendo ili tuendelee kulinda amani ya nchi yetu, na katika swala la upendo tunatakiwa sisi kama viongozi wa kanisa pamoja na kanisa tuanze na sisi kupendana na kiwahimiza wananchi kudumisha amani tulionayo na ili taifa liwe na nguvu lazima tuenzi na kulinda amani tulionayo"alisema mchungaji Orche Mgonja kutoka kanisa la Pentekoste la lift him up.

Aidha pia viongozi hao wadini walimpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli pamoja na mkuu wa wilaya ya Arumeru  Jerry cornel Muro kwa jinsi wanafanya kazi na kuwajali wananchi wa chini pia waliwapongeza serikali ya magufuli kwa jinsi wanavyowaheshimu viongezi wa dini. 

No comments:

Post a comment