Monday, 6 May 2019

Taarifa rasmi ya CHADEMA juu ya Mdude Nyagali kuchukuliwa na wasiojulikana

Jana May 5, 2019 CHADEMA katika hali ya dharura imesema inafatilia taarifa za Kijana Mdude Nyagali kuvamiwa na kuchukuliwa na wasiojulikana Ofisini kwake Mbozi Songwe.
Nainukuu taarifa iliyotolewa na Tumaini Makene ambeye ni Mkuu wa Idara ya Habari Mawasiliano “Yalikuja magari mawili wakashuka Watu wanne, alipiga kelele Wananchi wakajitokeza lakini Watu hao waliwatisha kwa bastola”
“Imedaiwa kuwa baada ya muda mfupi kulisikika purukushani, watu hao wakijaribu kumkamata Mdude huku wakimpiga na yeye akipiga kelele za kupinga kitendo hicho na kuomba msaada” Makene
“Tayari CHADEMA kupitia kwa Viongozi wa Chama katika eneo husika na Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga, kimevitaarifu vyombo vya dola Mkoani Mbeya, kwanza kutoa taarifa ya tukio hilo lenye mazingira ya utekaji pia kutaka kujua kama kuna askari waliopewa kazi ya kwenda kumkamata Mdude” Makene
“Hadi sasa haijulikani Mdude yuko wapi!, tupaze sauti zetu sote kulaani tukio hili na kutaka Mdude arudishwe au aachiliwe akiwa salama” Makene
Katika hatua ya sasa, CHADEMA kwa nguvu zote kinalaani vikali tukio hilo. Tunavitaka vyombo vya dola, hususan Jeshi la Polisi lenye wajibu wa kulinda raia na mali zao, kufuatilia taarifa za tukio hilo kama zilivyoripotiwa kwa polisi katika eneo husika na kuhakikisha Mdude anapatikana na wahalifu waliotenda tukio hilo wanajulikana, kukamatwa na kufikishwa mbele ya sheria” Makene

No comments:

Post a comment