Bunge wa Iringa Mjini, Mch. Peter Msigwa amehoji bungeni uhalali wa uamuzi wa Spika Job Ndugai kusimamisha uwakilishi wa Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele (CCM) katika Bunge la Afrika (PAP), bila Bunge la Tanzania kujadili kabla ya kufikia uamuzi huo.

Utakumbuka hapo jana Spika Job Ndugai alisema kuwa amemuandikia barua Rais wa PAP ya kusitisha uwakilishi wa Stehen Masele hadi Kamati ya Maadili itakapokamilisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake.

Spika alidai kuwa, "Katika uwakilishi wa Bunge la Afrika kumetokea matatizo makubwa hasa kwa Mhe.Steven Masele matatizo ya kinidhamu,Tumelazimika kumrudisha nyumbani kuanzia Jumatatu, badala yake amekuwa akionyesha kugoma, ni kiongozi ambaye anafanya mambo ya hovyo hovyo"
Share To:

msumbanews

Post A Comment: