Magari yagongana uso kwa uso, wawili wahofiwa kufa


Watu wawili wanahofiwa kufariki dunia baada ya gari ndogo lenye namba za usajiri T 340 DHG kugongana uso kwa uso na Fuso katika eneo la Mdaula mkoani Pwani.

Taarifa za awali kutoka kwa mashuhuda zinadai kwamba, waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea lea majira ya asubuhi walikuwa katika gari dogo. Dereva wa Fuso na abiria wake wamekimbizwa katika hospitali ya Chalinze kwa matibabu zaidi.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: