Thursday, 9 May 2019

Dkt. Mengi alikuwa kielelezo halisi cha mtu anayechukia umasikini - Lowassa


Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametoa salamu za rambirambi kwa kifo cha Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi akielezea kuwa alikuwa kielelezo cha mtu aliyechukia umasikini.

Lowassa ametuma salamu zake hizo kupitia Aboubakary Liongo ambaye ni msemaji binafsi wa mwanasiasa huyo akieleza ni majonzi makubwa kumpoteza kaka na rafiki kwake.

"Dkt. Mengi alikuwa kielelezo halisi cha mtu anayechukia umasikini kwa vitendo na kuishi maisha yake kuwanyanyua wengine katika kuupinga umaskini.” ameeleza.

Amendelea kwa kusema, "Umekuwa na mchango mkubwa sana katika maendeleo ya taifa letu na watu wake. Umeacha alama kubwa ya upendo, moyo wa kutoa na unyenyekevu kwa jamii alama ambayo Watanzania tutakukumbuka nayo daima. Lala salama kaka,”.

No comments:

Post a Comment