Friday, 3 May 2019

Baadhi ya akina mama wajawazito hupoteza maisha kwa kuchekewa kifika vituo vya Afya


Mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka akizungumza Wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze Tuwavushe salama ilyofanyika mkoni hapo.
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi wa Jiongeze tuwavushe salama iliyofanyika mkoani Simiyu.
Wadau wakiwa katika uzinduzi wa Kampeni ya Jiongeze tuwavushe salama Mkoani Simiyu.

Na.Vero Ignatus.

Baadhi ya akina  mama katika Halmashauri ya mji Bariadi hawana maamuzi ya kwenda hospitali kupata huduma za afya, wakisubiri ruhusa kutoka Kwa waume wao au wakwe zao.

Hayo yamesemwa na  Mratibu wa Afya ya Mama na Mtoto katika halmashauri ya Mji wa Bariadi, Frida Buyoga katika uzinduzi Wa kampeni ya ' Jiongeze Tuwavushe Salama katika mkoa wa Simiyu, amesema ukosefu huo wa kutoa maamuzi umepelekea wengi wao kupoteza Maisha Kwa sababu ya kuchelewa kufika vituo vya Afya.

Ukosefu wa maamuzi pia unapelekea baadhi ya akina mama hao  kushindwa kupanga uzazi wa mpango mpaka wawaulize waume zao.

 Buyoga,  amesema hali hii imepelekea vifo vya vya akina mama 14 , kati ya 120 waliochelewa kufika vituo vya afya kwa sababu mbalimbali mwaka jana.

Licha ya akina mama hao kufariki, watoto wao waliokuwa bado hawajazaliwa (tumboni)  walikutwa hawachezi (wamefariki) baada ya kuchelewa kufika vituo vya Afya.

Amesema miongoni mwa sababu nyingine zinazopelekea baadhi ya akina mama  kuchelewa kufika vituo vya Afya ni pamoja na umbali Wa baadhi ya  vituo vya Afya, ambapo baadhi yao hulazimika kusafiri hadi kilometa 30 kwenda katika vituo vya Afya.

" Jitihada Kubwa zimefanyika kusaidia wajifungue Salama, ikiwemo ujenzi Wa zahanati na vituo vya Afya unaofanywa na serikali na wadau wa maendeleo.

Amesema katika halmashauri ya mji wa Bariadi, akina mama wastani 15-22 wanajifungua kila wiki , ikiwa ni ongezeko Kwa wanaokwenda kujifungua katika vituo vya Afya.

Baadhi ya akina mama wamekuwa wakijifungua Nyumbani, lakini baada ya kuwapa elimu, wengi wao sasa hivi wanakwenda vituo vya Afya kujifungua na kupata huduma Kwa ajili yao na watoto wao, anasema Buyoga.

Amesema uzinduzi Wa kampeni ya 'Jiongeze Tuwavushe Salama' utasaidia sana kuelimisha akina mama kwenda katika vituo vya Afya, kujua Afya zao na kufuatilia chanjo zote muhimu, ili kujilinda wao na watoto wao.

No comments:

Post a Comment