Tuesday, 30 April 2019

Yatakayojiri katika ziara ya Rais Magufuli leo MbeyaRais John Magufuli leo anaendelea na ziara yake mkoani Mbeya ambapo atahutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa John Mwakangale Mjini Kyela.

Pia ataweka jiwe la Msingi la ujenzi wa nyumba za walimu, mabwenu na maabara katika Chuo cha Ualimu Mpuguso na kuzungumza na wananchi wa Tukuyu.

Katika ziara yake siku ya jana Rais Magufuli alifungua kiwanda cha maparachichi wilayani Rungwe, mkoani humo, kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya lami ya Katumba – Mbambo – Tukuyu na ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya lami ya Kikusya – Matema.

No comments:

Post a Comment