Monday, 29 April 2019

SERIKALI YAZINDUA MAABARA YA TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA.

Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza, katika mkutano wa Pili wa Pamoja wa Mtandao wa Vyombo vya Udhibiti wa Nyuklia kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Aprili 29, 2019. 
 
Majaliwa, akisalimiana na Meneja Muandamizi wa Kituo cha Kimataifa cha Sayansi na Teknolojia na Mshauri wa Masuala ya Kidiplomasia (ISTC), Dkt. Kamen Velichkov, baada ya kufungua mkutano wa Pili wa Pamoja wa Mtandao wa Vyombo vya Udhibiti wa Nyuklia kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Aprili 29, 2019.
                              Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe wakati alipozindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.
 
Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akiweka jiwe la msingi, wakati alipozindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.
 
Majaliwa, akioneshwa kifaa cha kupimia mionzi na Mkurugenzi wa Kinga ya Mionzi, Dkt Firm Banzi, baada ya kuzindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.
 
Majaliwa, akioneshwa kifaa cha kupimia vifaa vya kupimia mionzi na Mkurugenzi wa Kinga ya Mionzi, Dkt Firm Banzi, baada ya kuzindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.
 
Majaliwa, akimkabidhi cheti na pesa kwa kutambua uaminifu wao kwa Mtafiti wa Mionzi Daraja la Pili, Machibya Matulanya baada ya kuzindua Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.
 
Majaliwa, akizungumza na wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi wa Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Aprili 29, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

No comments:

Post a comment