Thursday, 25 April 2019

RC Mtwara awataka waliokusanyika kujinusuru na kimbunga kurejea makwaoMkuu wa Mkoa wa Mtwara G.Byakanwa amewataka Wananchi waliokusanyika sehemu zilizotengwa na Serikali kujinusuru na kimbunga 'Kenneth' kurejea makwao na kuendelea na shughuli kwani uwezekano wa madhara kama ilivyotangazwa umepungua kwa kiasi kikubwa.

RC amewataka wananchi hao kuendelea na shughuli zao baada ya kujiridhisha na kupungua kwa kasi ya upepo wa kimbunga Kenneth huku wakiendelea kufuatilia taarifa za hali ya hewa sambamba na kuchukua tahadhari.

No comments:

Post a comment