Saturday, 13 April 2019

RC Makonda kumpa zawadi Golikipa wa Simba SCMkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemuahidi zawadi golikipa wa Simba Aishi Manula pindi watakaporejea nchini kutokana na kazi kubwa aliyoifanya leo nchini DRC kwenye mchezo wa leo wa robo fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika.

Mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliowakutanisha TP Mazembe na Simba SC umemalizika kwa TP Mazembe kufanikiwa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya Mabingwa Afrika.


"Najua matokeo ya leo yatatupa tabu sana mtaani ila wewe umekuwa nyota wangu ukifika tu DSM njoo uchukue zawadi yako. Watani zangu Naomba mjuwe hatua tuliyofikia ni kubwa sana na hakika Simba inastahiri kupongezwa na Usku nitakuwepo Airpot kuwapokea Makamanda na wapambanaji wetu Simba," ameeleza RC Makonda.

TP Mazembe wakiwa nyumbani kwao DC Congo wamuibuka na ushindi wa goli 4-1.Simba SC ndio walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Emmanuel Okwi kunako dakika ya pili, TP Mazembe
walisawazisha goli hilo dk ya 22 kupia Kabaso Chongo. Magoli mengine ya TP Mazembe yamefungwa na Meschack Elia, Trésor Mputu na Jackson Muleka

No comments:

Post a comment