Monday, 29 April 2019

Picha: Maboresho ya Mawasiliano ya simu Mji wa Serikali yaanza

Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na Mratibu wa Ujenzi wa Mji wa Serikali, Bw. Meshach Bandawe akielezea jambo kwa wawakilishi wa Kampuni za Simu za TTCL, Airtel, Tigo na Vodacom wakati wa ziara ya kukagua maeneo yatajayojengwa Minara ya Mawasiliano ya Simu katika Mji wa Serikali ikiwa ni mkakati wa kuboresha miundombinu ya Mawasiliano ya Simu katika mji huo na maeneo jirani


Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na Mratibu wa Ujenzi wa Mji wa Serikali,, Bw. Meshach Bandawe akiteta jambo na Mkuu wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Albert Richard wakati wa ziara ya kukagua maeneo yatajayojengwa Minara ya Mawasiliano ya Simu katika Mji wa Serikali ikiwa ni mkakati wa kuboresha miundombinu ya Mawasiliano ya Simu katika mji huo na maeneo jirani. Ziara hiyo imehusisha wawakilishi kutoka Kampuni za Simu za TTCL, Airtel, Tigo na Vodacom ambapo Kampuni zote zitakuwa zinatumia mnara moja. Katikati ni Fundi Sanifu wa Kampuni Ujenzi ya Gopa iliyopewa Kandarasi ya ujenzi wa Mnara wa Awali unaojengwa katika eneo hilo, Bw. Charles Mndilila
No comments:

Post a comment