"Wanasiasa tutumie majukwaa ya kisiasa  kwa weledi na umakini mkubwa  kuwaelimisha wananchi umuhimu wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwani jambo hilo limegusa maisha ya watu na manufaa ya pande mbili , kuvurugika kwake kuna gharama na hasara nzito"  Shaka

"Muungano uliodumu kwa miaka 55 tokea Mwaka 1964 , hauna budi kulindwa, kudumishwa na kuendelezwa, tokeo lolote la kuvurugika kwake, litahatarisha mahusiano, usalama na maisha ya watu ambao hawajui wala hawakuona ukoloni" Shaka

"Wanasiasa wanaotumia Muungano kama mtaji wa kujitafutia umaarufu ili  waungwe mkono na wananchi, viongozi hao wanahitaji kuepukwa ili kukwepa madhara mapema" Shaka

"Muungano wa Tanganyika na Zanzibar licha ya kuwa na  nia njema, udugu, asili , unadumisha mila na jadi za wananchi wake , umebeba  maisha ya watu zaidi ya milioni 55 baada ya miaka 55 kupita tokea kuundwa kwake" Shaka

 "Ulikuwa ni Muungano uliowaunganisha watu milioni 12 kwa iliokuwa Tangnyika na laki tatu wa Zanzibar mwaka 1964, bali sasa 2019  umebeba dhamana na usalama wa watu zaidi ya milioni 55 ambao hawatambui ukoloni, hawakuona uhuru 1961 wala Mapinduzi ya Zanzibar 1964" Shaka

"Wanasiasa waache kutumia kasoro ndogo ndogo zilizopo katika Muungano kusaka kiki za kisiasa , Muungano ni jambo nyeti linalobeba maisha na usalama wa watu. Kuna wananchi ambao hawakuona ukoloni bali wanatambua Muungano. Wamezaliwa na kujikuta wakiwa huru na wamoja kwa miongo kadhaa " Shaka

 "Wanaotumia dosari za Muungano kwa lengo la kufikia malengo yao kisiasa au kufikia matlaba, vyeo na madaraka, waache mchezo huo kwani masihara yao yanaweza kuleta misiba na majuto iwapo ndimi zao hazitachuja ya kusema na kujua ya kuacha" Shaka.

"Vinywa vya wanasiasa viwe na ashakum ya kuchagua maneno, midomo yao isibomoe kuta zinazolinda Muungano bali zijenge dhamira njema . Midomo yao isiwe njiti za kiberiti karibu na mapipa ya petroli, zisitoe cheche na moto, Muungano huu  una maisha ya watu na usalama wao" Shaka

"Ikiwa kuna watu bado wanafikiri muungano huu ni wa faida kwa kina Marehemu Mwalimu Julius Nyerere na hayati Sheikh Abeid Karume au kwa TANU na ASP huo ni mtazamo hasi, Muungano umekusanya watu wa makabila tofauti, dini, mila, desturi na maisha yao kwenye mikoa yote" Shaka

"Anayesaka madaraka na asake kivyake ila asichezea Muungano. Tubishane, tulumbane na kutaniana kwa mambo mengine bila kudhihaki Muungano. Muungano ukivurugika utaondoka na umoja, amani na utulivu . Bei za kujenga mahusiano mapya, uhusiano mwingine na mshikamano mpya ni ghali mno" Shaka

"Wanasiasa ndiyo walioisababishia Muungano wa Libya na Misri kuvunjika mapema, Muungano wa Ghana na Guenea, Senegal, Gambia na Mali ukavurugika huku watu wa aina hiyo ndiyo wakasabisha Ethiopia kugawanyika na baadae wakaivuruga Sudan zikatokea nchi mbili" Shaka

"Wanasiasa wa Tanzania na Afrika tujifunze kutoka Mataifa ya Ulaya na Marekani ambayo kufikia kwao mahali yalipo sasa kiuchumi na kimaendeleo, kumetokana na historia ya mataifa hayo kukataa kugawanyika na kuamua kuungana" Shaka

"Uingereza, Ujerumani na Marekani ni Mataifa yenye asili ya Muungano kihistoria. Wanasiasa wake wanazumgumza mengine katika mustakabali wao bila kuhatarisha miungano yao" Shaka

"Marekani hutashuka chini ya jukwaa mtu mmoja ukihamasisha nchi moja ijitoe katika Muungano wa nchi zao 52" Shaka

 "Tunapongeza juhudi za marais Dk John Pombe Magufuli na Dk Ali Mohamed Shein kwa umakini na umahiri walionesha katika kulinda na kuutetea muungano wa Tanzania katika uongozi wao" Shaka

" Dk Magufuli na Shein wanastahili pongezi nyingi katika jambo hili niendelee kuwahamasisha na kuwashajihisha wananchi na viongozi wengine wenye dhamana katika serikali zetu kuendelea kuzishughulikia kero na matatizo yote ya Muungano ili kupata utatuzi kabla hawajawapa maneno wanasiasa uchwara wanaotaka kuutumia dosari za muungano kama mradi wa kuwagawa watu wakati ni jambo hatari"  Shaka

Hii ni sehemu ya mahojiano ya Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumza na Mwandishi wa Mtanzania kuelezea maoni yake juu ya miaka 55 ya Muungano wa Tanzania  26 April 2019
Share To:

msumbanews

Post A Comment: