Waziri Nchi,Ofisi yaMakamu wa  Rais, Anayeshughulikia  Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba akizungumza katika mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika leo jijini Dodoma katika ukumbi wa hotel ya Morena

Na.Vero Ignatus ,Dodoma 
Mkutano mkuu wa Mabadiliko ya Tabianchi umefanyika leo Jijini Dodoma ukiwashirikisha wadau zaidi ya 100 wameshiriki katika mkutano huo ukiwa na lengo la kujadili mabadiliko ya Tabia nchi na kujikwamua katika taizo hilo kama Taifa

Akifungua mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa FORUMCC Eric Mugurusi amesema lengo kuu la mkutano huo ni kujadili Sera ambazo zitatilia maanani mabadiliko ya Tabia nchi na namna ambavyo wananchi watashirikishwa ili kupunguza athari za mabadiliko hayo.  

 Amesema kuwa mkutano huo ni maalum kwaajili ya kuona nam,na ambavyo sera zinavyoweza kuwaondoa kwenye tatizo hiolo na ushirikiswahwaji wa wananchi katika hayo yote.

Waziri Nchi,Ofisi yaMakamu wa  Rais, Anayeshughulikia  Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba akizungumza katika mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi
amesema katika kuhakikisha tunaondoa tatizo la mabadiliko ya tabia nchi kuwajumuishe watu wote,  kujifunze katika nchi zilizofanikiwa na kuzitumie mbinu hizo, Kuaanda Sera nzuri,Kuwahimiza watunga Sera kuamuru uchukuliwaji wa hatua

Mhe.Makamba amesema kuwa kwenye baadhi ya nchi Mabadiliko ya tabia ya nchi yametangazwa kama usalama wa nchi ambapio nasi kama nchi ipo haja ya kuonesha kuwa changamoto zinaweza kuwa kubwa kwani Utalii wetu ni Fukwe ambazo zinalika na thamani yake inaondoka sababu ya mabadiliko ya tabia ya nchi,hivyo utalii unapotea.

"Mama  yangu alikuwa Nesi miaka ya 1980 anasema kipindi hiko hakukuwa kabisa na kesi za wagonjwa wa malaria, lakini angali miaka ya sasa,Wagonjwa wa malaria wamekuwa wengi na ndo ugonjwa mkubwa hii ni sababu ya ongezeko la Mbu kwa kasi kubwa na kutokutunza mazingira yetu”Alisema Makamba

  Amesema kati ya miaka 5-10 mabadiliko ya tabia nchi yalionekana kama nadharia au yanawahusu wanasayansi ila kadri siku zinavyozidi kwenda ndivbyo tatizo linavyozidi kuwa kubwa, hata kwenye kilimo sababu ya mabadiliko ya Majira kumesababisha kuchelewa kwa mvua hivyo Kilimo kinafanyika kwa shida  pia yanapelekea umasikini.

Mimi nilisomeshwa sana kwa kilimo cha Chai na Kahawa ambacho ndio kikubwa Tanga, lakini sasa hivi kilimo cha mazao haya kinapotea,hali hii ni ishara ya kuongezeka kwa umasikini''Alisema Makamba

Kwa upande wake Meneja Mradi kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Oxfam Jovita Mlay amesema kuwa Mabadiliko ya Tabianchi yanaongeza umasikini kwa wanawaume na wanawake lakini wahanga wakubwa zaidi ni wakina mama na watoto kwani inagusa maeneo ambayo wanawake wanajipoatia kipato napo no kwenye kilimo.

Amesema kuwa wakati wa kushughulikia majanga kama hayo ni muhimu kuhakikisha kuwa inawekwa mipango na usimamizi wa kisera unaoweza kupunguza na kumaliza madhara ya yatokanayo na mabadiliko ya Tabianchi kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali

Amesema Oxfam inaendelea kufanya kazi  ili kuhakikisha kuwa maswala yanayoingizwa katika mipango mikakati na kuendelea kusapoti juhudi zinazofanywa na wadau katika kupambana na mabadiliko ya Tabianchi.

Kwa upande wake mbunge wa Babati vijijini Mhe,Jitu Soni amesema kuwa jamii nyingi zinaishi katika mazingira magumu kutokana na mabadiliko ya Tabianchi amesema kuwa mabadiliko hayo siyo jambo la mazingira peke yake bali linahusisha maswaka ya uchumi,miundombinu,mifumo ya uzalishaji,rasilimali,na nishati.

Nae Mwenyekiti wa Bunge ya Bajeti na mbunge wa Kibakwe Mhe.George Simbachawene amesema kuwa mgawanyo wa shughuli za kibinadamu imekuwa sababu kubwa ya uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya Tabianchi,amesema bado elimu inahitajika zaidi katika jamii zetu haswa vijijini ili kujinasua katika tatizo hilo.

Aidha watu wengi wanaharibu mazingira kwasababu ya kutafuta maji na nishati,uwekezaji wa kutafuta maji unatumia gharama kubwa sana,amesema nchi inahitaji kutengeneza mfumo wa kitaalam katika uharibifu wa mazingira kwani hali ni mbaya sana 

Mshiriki kutoka Asasi za kiraia mkoa wa Kagera bi Zainabu Shakiru amewaomba Serikali pamoja na wadau kuwa mchakato wa utekelezaji wa sera ya mabadiliko ya tabianchi wananchi nao washirikishwe ipasavyo ili waweze na wao kuitambua sera hiyo
Akifungua mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa FORUMCC Eric Mugurusi amesema lengo kuu la mkutanowa tano wa mabadiliko ya tabianchi Jijini Dodoma leo
Meneja Mradi Jovitha Mlay kutoka Shirika la Oxfam akizungumza katika mkutano wa tano wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika leo Jijinj Dodoma katika hotel ya Morena
Washiriki wa mkutano wa tano wa mabadiliko ya Tabianchi Jijini Dodoma leo
Ndugu Jensen Shuma kutoka shirika la TaTEDO akichangia mada katika mkutano wa tano wa mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Jijini Dodoma
Dkt.Lucy Ssendi Mshauri wa Maswala ya Mabadiliko ya Tabianchi ,Mradi wa Decentralized Climate Finance -TAMISEMI akichangia mada katika mkutano wa Tano wa mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Jijini Dodoma

Makamu Balozi wa EU Nchini Tanzania Charles Stuart akizungumza na washiriki wa mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi Jijini Dodoma leo.

Jovita Mlay Meneja wa Mradi kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la Oxfam Tanzania akizungumza katika mkutano wa mwaka wa mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika leo Jijini Dodoma katika hoteli ya Morena
Washiriki kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini Tanzania waliohudhuria katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Jijini Dodoma katika Hotel ya Morena.
Mkurugenzi mtendaji wa Jumuiko la maliasili Tanzania( TNRF)Zakaria Faustin akizungumza katika mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Jijini Dodoma.
Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: