Friday, 19 April 2019

Majambazi wamuibia Mkuu wa WilayaJeshi la Polisi Mkoani Mtwara limesema wezi wameingia nyumbani kwa mkuu wa wilaya ya Mtwara Evodi Mmanda usiku wa Aprili 16, na kufanikiwa kuiba Tv Bapa.

Akieleza matokeo ya oparesheni inayotekelezwa na jeshi hilo, kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Blasius Chatanda, amesema wezi hao hawakufanikiwa kuondoka na vitu vingine vya ndani mbali na TV hiyo.

"Watuhumiwa walioshiriki tukio hilo tayari tunao, kulikuwa na ulinzi na kukatokea tukio ndio maana
nikasema uchunguzi unaendelea kujua kilifanyika nini mpaka hili likatokea," ameeleza.

Ameendelea kwa kusema,'Kama kulikuwa na mlinzi halafu hakuzuia hilo tukio hadi linatokea kwa
utaratibu hatua zinachukulia dhidi ya aliyekuwa analinda'.

No comments:

Post a comment