Monday, 22 April 2019

Madawa ya kulevya yakamatawa Mererani
Na John Walter-Manyara

Polisi mkoani Manyara wamewakamata watu 2, kwa makosa ya kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya ambayo kwa Tanzania ni kinyumke cha kisheria .

Akitibitisha kukamatwa kwa madawa hayo kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Augustino Senga amesema, huko katika wilaya ya Kiteto amekamatwa Ramadhani Kombo  mwenye umri wa  miaka 20 akiwa na Kete 24 za Bangi wakati anapekuliwa ili kuingizwa mahabusu  kwa kosa la uvunjaji ikiwa ni kosa la lingine la aina hiyo kwa mtuhumiwa huyo.

Aidha katika mji mdogo wa Mirerani katika geti la kuingilia kwenye machimbo ya Tanzanite wakati wa upekuzi wa kawaida walimkamata Jacob Ngoti mwenye umri wa miaka 43 akiwa na misokoto 1248 yenye uzito wa kilogram 2.740 akiwa ameiweka kwenye begi  la nguo la mgongoni ili asiweze kugundulika kirahisi.

Madawa hayo, alikuwa anakwenda kuwauzia wachimbaji wanaofanya kazi za uchimbaji ndani ya Ukuta wa Madini maarufu kama ukuta wa Magufuli.

Kamanda wa Polisi Augustino Senga amesema kuwa jeshi hilo lipo makini na halitamvumilia mtu yeyote anaejishugulisha na uuzaji au utumiaji wa madawa ya kulevya.

No comments:

Post a comment