Saturday, 27 April 2019

Jambo usilolijua kwenye wimbo mpya wa Alikiba


April 26, 2019, Msanii wa Bongo Fleva, Alikiba ameachia video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Mbio.

Muda mfupi baada ya kuachia wimbo huo, Alikiba ameeleza siri nzito iliyopelekea kuachia wimbo huo hivi sasa.

Alikiba amesema kuwa wimbo huo aliuandika takribani miaka 10 iliyopita aliposafiri kwa mara ya kwanza nchini Oman.

"Allow me to introduce to you MBIO ngoma ambayo niliandika miaka 10 iliyopita nilipokwenda Oman 🇴🇲 kwa mara ya kwanza, miaka 10 baadae niliporudi Oman kwa ajili ya concert yangu kubwa at Intercontinental Hotel, I got inspired to finalise the song na kushoot Music Video in Muscat.
"
Mara ya mwisho kwa Alikiba kutoa wimbo wa peke yake ni takribani miezi minne iliyopita ambapo alitoa wimbo wa 'Kadogo'.

No comments:

Post a comment