Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii Mhe.Kinyerembe Lwota akizungumza katika Mkutano wa Mabadilikobya Tabianchi Jijini Dodoma
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Bajeti na mbunge wa Kibakwe George Simbachawene akichangia jambo katika mkutano wa mabadiliko ya tabianchi yaliyofanyika Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Forumcc Rebbecca Munna akichangia jambo katika mkutano waliouandaa wa mabadiliko ya tabianchi Jijini Dodoma katika hotel ya Morena

Mbunge wa Babati vijijini Mhe. Jitu Soni akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa mabaliko ya tabianchi uliofanyika Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala Tabu Shahibu akitoa ufafanuzi wa kile wanachokifanya katika halmashauri hiyo katika mkutano wa mabadiliko ya tabianchi Jijini Dododma
 Muwakilishi wa Mkurugenzi wa Singida Rehema akizungumza katika mkutano wa tano wa mabadiliko ya tabianchi Jijini Dodoma
Dr Ronald Ndesajo kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam akiwasilisha matokeo ya Tathmini ya Kijinsia na Madhara ya Mabadiliko ya Tabia Nchi

Na. VERO IGNATUS, DODOMA 

Serikali za mitaa nchini zimetakiwa kubuni miradi ya kupunguza hewa ya ukaa ,kilimo,misitu,na kutengeneza ajira kupitia shughuli hizo ambazo zina wajibu wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi maana wao ni watekelezaji wa sera.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii Mhe.Kinyerembe Lwota ambapo 52%ya uharibifu wa mazingira wa miti unafanyika katika halmashauri nyingi nchini   amesema asilimia 90 ya watanzania wanatumia mkaa majumbani kwao ni zaidi na huo ni uharibifu mkubwa zaidi ya  hekari laki 4 kwa mwezi 


Amesema upandaji wa miti unaofanyika kwa sasa haulingani na uharibifu uliofanyika amesema upandaji wa miti unahitajika ufanyike kwa wingi kulingana na matumizi yaliyofanyika amesema wao kama kamati ya bunge wanaomba gesi ipungue bei ili wanancgi waweze kutumia hiyo swala la miti na mikaa itapungua kwa kiasi kikubwa 


“Kamati ya bunge ya Ardhi,maliasili,utalii tulifanya ziara katika ziwa manyara hali ya lile ziwa ni mbaya kabisa ukiangalia tunakoelekea ziwa lile linakwenda kukauka kabisa ,baada ya hapo tulitoa ushauri na tumeona hatua zinachukuliwa kwaajili ya kulinusuru kwasababu utalii wetu ni wawanyama na wanyama wanapata maji na malisho katika ziwa hilo”.Alisema Kinyerembe


Amesema jambo lingine walilolifanya kama kamati ni kuishauri serikali TFS kuwa Mamlaka kamili kwani kwa sasa haina mamlaka ya kufanya shughuli hizo kwa mapana zaidi kwani uwajibikaji wa moja kwa moja haupo ila itakapokuwa mamlaka ni rahisi kuwabana 


Kwa upande wake mkurugenzi wa FORUMCC amesema kuwa swala la upatikanaji wa taarifa sahihi wa mabadiliko ya tabianchi haswa maeneo ya vijijini wana elimu duni juu ya mabadiliko ya tabianchi ,amewataka wanahabari kuhakikisha wanaandika taarifa amabazo zitawafikia watu wa vijijini


Amesema ukulima isiwe ndiyo sababu ya uharibifu wa mazingira tufanye kilimo chenye tija na maslahi kwetu na vizazi vijavyo vije kufaidika kwa kukuta mazingira mazuri nah ii lazima tutunze mazingira yetu.alisema Rebecca.


Nawapa changamoto ya kila mmoja kutokuwa muhudhuriaji tu wa semina lakini pia wawe watendaji. Nashukuru sana wote tulioshirikiana nao wakiwamo OxfamTz na timu nzima ya vijana wa mitandao ya kijamii. Mhe. JMakamba amekuwa anatoa sana sapoti katika posti zetu. 


Mkurugenzi wa Halmashauri  ya Ilala Tabu Shahibu amesema kuwa kwenye eneo la mazingira wametoa elimu katika shule za msingi ambapo wanafunzi wanaelewa namana ya kulinda na kutunza mazingira ,amabapo amesema kuwa wamepiga kelele kuhusiana na utupaji wa taka hovyo na kwa sasa wanaelekea kwenye shule za sekondari.


Amesema Halmashauri hiyo imefanya kazi ya kuwajengea uwezo madiwani ili kuhakikisha kuwa wanatengeneza sharia mbadala kwenye serikali za mitaa ili kulinda mazingira 

,mabadiliko ya tabianchi ambayo kwa sasa mabadiliko hayo yanaathiri watu wengi

Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Ufugani na Maji na mbunge wa Babati vijijini Mhe. Jitu Soni amesema kuwa anatamani Halamashauri zote, vijiji, tarafa, wilaya hata mikoa iwe na mashindano ya kutunza mazingira. 


Amesema hiyo italeta motisha mkubwa katika jamii na eneo husika hakuna atakayekubali kuwa wa mwisho katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama 


Kaya moja ikiwa inatumia kuni na mkaa kwa miaka 10 wanakuwa wameteketeza ekari zaidi ya 30 Je Ni Watanzania wangapi wanapanda miti ya kutosha? Tunalikaribisha jangwa ~ Frank Luvanda kutoka SUHOLE foundation Morogoro 




Dr Ronald Ndesajo kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam akiwasilisha matokeo ya Tathmini ya Kijinsia na Madhara ya Mabadiliko ya Tabia Nchi na Uwezo wa Kukabiliana Nayo kwa Miradi ya Ardhi Yetu Programme(AYP II) na HELP Katika hali ya kawaida, Kilimo kimepatwa na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi 

Ndesanjo amesema kutokana na changamoto hiyo, kwa asilimia kubwa  Wanawake wamepatwa na changamoto kwa kiasi kikubwa,Pili Wanawake ndio wanaoshughulika na shughuli za kila siku nyumbani ; Upatikanaji wa maji tabu sana 
Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: