Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (kushoto) akisalimiana na Binti Mfalme wa Jordan Sarah Zeid wakati wa ziara yake Nchini kukagua miradi ya Lishe inayotekelewa na Shirika la Chakula Duniani (WFP).
  Binti Mfalme wa Jordan Sarah Zeid akizungumza na WaziriwaNchi OR- TAMISEMI Mhe. SelemaniJafo (Mb) wakati wa ziara yake nchini kukagua miradi ya Lishe  inayotekelewa na Shirika la Chakula Duniani (WFP).
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani Michael Dunford akizungumza wakati wakikao

1.     Waziriwa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (katikati) akiwa na Binti Mfalme wa Jordan Sarah Zeid(kushoto) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la ChakulaDuniani Michael Dunford
Katika  Picha ya Pamoja ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na S erikali za  Mitaa Mhe. Selemani Jafo (katikati) akiwa na Binti Mfalme wa Jordan Sarah Zeid, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la ChakulaDuniani Michael Dunford pamoja na watalaamuwa OR-TAMISEMI pamoja na WFP

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amelitaka Shirika la ChakulaDuniani (WFP) kuendelea kutoa ushirikiano katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ili kuendelea kuboresha masuala ya Lishe katika jamii.
Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa kikao na Binti Mfalme wa Jordan Sarah Zeid cha kujadili masuala mabalimbali yanayohusiana na Lishe sambamba na miradi inayofadhiliwa na fedha za Umoja wa Ulaya kupitia  Shirika la chakulaDunia.
Waziri Jafo aliwashukuru kwa ushirikiano wanaowapatia katika miradi mbalimbali ya Lishe na hakika wamekua na mchango mkubwa katika kuboresha Lishe Tanzania Kwa kuwa Lishe ni suala endelevu na mtambuka wanaomba wa endelee kutoa msaada zaidi  wakifedha na kitaalamu ili Lishe izidi kuboreshwa katikajamii.
‘HatuwezikufikiaTaifa la Uchumiwa Kati endapowatuwetuhawatakuwanalishe bora, iliwatuwafanyakazikwabidii, waweze kuzalisha nakulipa kodi inavyotakiwa  nilazima wawe naAfya bora wakati wote hivyo kuendele akutoa      elimunakuhamasishalishe bora nivitumuhimu sana katika kufikia lengo la Kitaifa” alisema Mhe. Jafo.
Katika kikao hicho Mhe.Jafo alizungumzia suala la kuanzisha Siku ya Lishe kitaifa itakayoazimishwa kila mwaka ili kuendelea kutoa Elimu kwa Umma kuhusu umuhimu wa Lishe katika maisha ya kila siku yamtanzania.
Alimtaka Binti Mfalme wa Jorda Sarah Zeid kuendelea kutoa ushirikiano katika kufanikisha siku hii muhimu ya kitaifa itakayoanza kuazimishwa mwaka huu wa 2019.
Naye Binti Mfalme Sarah Zeid amesema amefurahishwa sana na utekelezaji  wa miradi ya Lishe inayotekelezwa katika Halmashauri nne Nchini na ameridhishwa na matokeo aliyoayaona kuptia miradi ya wananchi.
Ameahidi kupitia Shirika la Chakula Duniani (WFP) kuendelea kutoa ushirikiano katika miradi mingine itakayoendelea kutekelezwa ilik uhakikisha Lishe inaboreshwa katika Jamii.
NayeMwakilishi Mkaazi waShirika la ChakulaDuniani Michael Dunford amesema watashiriki kikamilifu katika kuadhimisha siku ya Lishe Kitaifa na watatoa ushirikiano unaohitajika katika kufanikisha siku hiyo.
Shirika la ChakulaDuniani (WFP) linaratibu mradi wa Boresha Lishe unaotekelezwa katika Halmashauri nne Nchini ambazo ni Bahi, Ikungi, Singida Dc pamoja na Chamwino.
Share To:

Post A Comment: