Na Vero Ignatus, Arusha

KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel ameagiza halmashauri zote nchini kutoa elimu kwa wafugaji umuhimu wa utumiaji mbegu bora zinazozalishwa kituo cha Taifa cha Uhimilishaji mifugo kwa njia ya chupa NAIC kilichopo Wilayani Arumeru,Mkoani hapa.


Ametoa agizo katika  ziara ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji, ambapo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, ambapo Prof.Gabriel amesema ni kufuatia uwepo wa mwamko mdogo wa wafugaji katika utumiaji mbegu hizo.

Amesema kuwa ili kuendana na uchumi wa viwanda ni lazima wafugaji nchi wabadilike na kutumia mbegu hizo ili kupata Ng'ombe wenye nyama bora,maziwa,ngozi na Kwato watakazokidhi malighafi za viwanda.

Prof.Ole Gabriel amesema  kwa kipindi cha mwaka jana waliweza kutoa mafunzo kwa wafugaji 58,000 kwa nchi nzima hali iliyosababisha kuzalisha Ndama 10,000 pekee licha ya kituo hicho kuzalisha mbegu 60,000 kwa wiki.

"Idadi ya wagufaji waliopewa elimu ni ndogo na mwitikio wa utumiaji mbegu hizi hauridhishi kwa wafugaji wetu wakati kituo kinazalisha mbegu za kutosha kwa mahitaji ya wafugaji wote nchini,hivyo nawaagiza wataalamu wote watoke ofisini waende kwa wafugaji kutoa elimu juu ya utumiaji mbegu hizi,"alisema

Aidha alitumia nafasi  hiyo kuwataka wafugaji kuondokana na dhana potofu kwakutumia mbegu hizo ni kuharibu vizazi vya ng'ombe jambo ambalo sio sahihi ni kukinzana na maendeleo katika sekta ya ufugaji. 

Kwa upande wake  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega kuwa hali ya usambazaji wa mbegu hizo kwenye vituo vilivyopo kanda saba nchini hauridhishi kutokana na baadhi ya waataalamu kutotimiza wajibu wao wa utoaji elimu kwa wafugaji.

"Serikali inauza mbegu hizi kwa ruzuku ili wafugaji wasiokuwa na uwezo waweze kumudu gharama ya Sh.5000,lakini kuna baadhi ya wataalamu wananunua mbegu hizi na kuziuuza kwa bei kubwa kati ya Sh.15,000 na Sh.40,000,"alisema

Ametoa wito kwa wafanyabiashara binafsi wa mbegu za chupa kuacha kuagiza mbegu hizo nje ya nchi na kuuzia wafugaji mbegu hizo kati ya Sh.50,000 hadi 100,000.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bungeya Kilimo,Mifugo na Mjai,Mahmoud Mgimwa alisema utumiajo wa mbegu hizo utawezesha wafugaji kufuga kwa tija na kupata soko la uhakika la bidhaa za mifugo yao.

"Kikubwa hapa wafugaji wabadilike kutoka kwenye ufugaji wa maea na kufuga kisasa kwa kutumia mbegu hizi za NAIC ili tushiriki uzalishaji wa malighafi za Viwanda vyetu vinavyoanzishwa kwa wingi nchini,"alisema.

Hadi sasa kiruo hicho kina madume 28 ya aina zofuatavyo katika kituo hicho NAIC
Ng'ombe wa maziwa Ayrshine 6,Friesian7 na Jersey 2.Ngombe wa maziwa na nyama (Dual porpose) Simmental 2 na Mpwapwa 4,Ng'ombe wa nyama, Boran 4 na Binsmara2 na Teaser bull 1.

Mwisho
KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel ameagiza halmashauri zote nchini kutoa elimu kwa wafugaji ili waweze kupata ngombe bora wa nyama, maziwa na ufugaji wenye tija

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na waandishi wa habari katika kutuo cha NAIC kilichopo Usariver Mkoani Arusha
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bungeya Kilimo,Mifugo na Mjai,Mahmoud Mgimwa
 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji waliotembelea katika kituo hicho kujionea jinsi uhamilishaji
Baadhi ya ng'ombe walipo katika kituo cha NAIC kwajili ya Uhimilishaji
Ngombe aliyeko tayari kwaajili ya Uhamilishaji katika kituo cha NAIC. Picha na Vero Ignatus. 
Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: