Wednesday, 27 March 2019

RC Makonda kuandaa semina kuhusu mirathi kwa wajane


Kufuatia kilio cha wajane wengi kunyanyasika na kuishi maisha ya tabu baada ya waume zao kupoteza maisha, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameandaa semina maalumu kwa ajili ya kuwajengea uwezo wajane inayotaraji kufanyika April mwaka huu.

RC Makonda amesema amefikia uamuzi huo baada ya kuona changamoto kubwa inayowakabiki kwenye suala zima la mirathi, malezi ya familia na kipato.

No comments:

Post a comment