Tuesday, 19 March 2019

Nassari amponza Mbunge mwingine wa CHADEMA

Spika wa Bunge anafikiria hatua za kinidhamu za kumchukulia Mbunge wa Kilombero Mhe. Peter Lijualikali kufuatia kauli za kejeli dhidi ya Bunge

Taarifa hiyo imeeleza kwamba  kauli hizo zimetolewa na Mbunge huyo siku ya jana, Machi 17, wakati akizungumza na wanahabari katika mkutano wa Joshua Nassari ambaye amevuliwa Ubunge wiki iliyopita.

Katika mkutano huo, Lijualikali alishangazwa na kitendo cha Spika kumvua ubunge Nassari wakati Mbunge huyo alipodai kuwa alitimiza wajibu wake wa kulitaarifu bunge juu ya matatizo anayopitia.

No comments:

Post a comment