PIC 01-min
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania, Anthony Mataka (wa pili kushoto) akimpongeza mshindi wa kwanza katika mbio za kilomita 21 maarufu kamaTigo Kili Half Marathon Emmanuel Giniki baada ya kuibuka mshindi. Wa kwanza kulia aliyeshikilia mfano wa hundi kwa ajili ya kumkabidhi mshindi huyo ni ni Mkurugenzi Mtendaji wa  Kamuni ya Tigo Simon Karikari
PIC 02-min
Baadhi ya Wafanyakazi wa Tigo wakiwa na nyuso za furaha huku wakionyesha medali zao baada ya  ‘kufuta vilimia’ na kufanikiwa kumaliza mbio za kilomita 21 maarufu kama Tigo Kili Half Marathon zilizofanyika mjini Moshi ambazo ziliwashirikisha wakimbiaji kutoka nchi zaidi ya 50 duniani
PIC 03-min
Mshindi wa mbio za Kilomita 21 maarufu kama Tigo Kili Half Marathon Emmanuel Giniki akihojiwa baada ya kufanikiwa kuibuka mshindi  wa kwanza katika mbio hizo zilizofanyika mjini Moshi na kuwashirikisha wakimbiaji kutoka nchi zaidi ya 50 duniani
PIC 04-min
Mkurugenzi Mtendaji Tigo Simon Karikari (wa kwanza kulia)akiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Rais wa RT Anthony Mtaka waki mkabadhili mfano wa hundi ya Sh milioni 1, 025,000 Falluna Abdi aliyeshika nafasi ya pili kwa wanawake kwenye mbio za Kilometa 21 maarufu kama Tigo Kili Half Maratahon zilizofanyika mjini Moshi.
……………………………
Na Mwandishi Wetu
MTANZANIA Emmanuel Giniki ameibuka mshindi wa mbio za kilomita 21 maarufu kama Tigo Kili Half Marathon zilizofanyika mjini MoshI.
Giniki amevunja mwiko kwa mbio hizo ambazo kwa miaka mingi zimekuwa zikitawaliwa na raia wa kigeni na husasani Wakenya ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakiibuka washindi.
Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni mbili, Giniki alisema anayofuraha kushinda mbio hizo na kuiletea heshima nchi yake jambo ambalo amekuwa akilitamani.
“Pamoja na kwamba mbio hizi zimekuwa zikifanyika hapa nyumbani, tumekuwa tukishindwa kuzitendea haki kwa kuwa wageni ndiyo wamekuwa wakizitawala. Ninayofuraha leo nimeweza kulitoa taifa langu kimasomaso,” alisema.
Akiongea wakati wa halfa ya kukabidhi zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Simon Karikari alisema kampuni yake inayofuraha kuchangia maendelea ya michezo nchini na hususani riadha ambayo pia huboresha afya
Karikari alisema Tigo imekuwa mdhamini wa mbio za Kili half Marathon kwa kipindi ch miaka minne mfululizo na kuongeza kuwa itaendelea kudhamini pamoja na kuboresha mbio hizo kila mwaka.
Waziri wa Habari, utamaduni vijana na Michezo Dk Harrison Mwakyemba aliishukuru Tigo kwa kudhamini mbio hizo na kuwataka wakazi wa Moshi kutumia fursa zitokanazo na mbio hizo kujijenga kiuchumi.
“Mbio hizi zimeleta wakimbiaji kutoka nchi zaidi ya 50 hapa mjini Moshi. Idadi hii kubwa ya watu itokanayo na mbio hizi ni fursa nzuri ya kibiashara na ni vyema wakazi wa Moshi wakaichangamkia,” alisema Waziri Mwakyembe.
Mbio za Kilimanjaro Marathon hufanyika mjini Moshi kila mwaka. Idadi ya washiriki wa mbio hizo imekuwa ikiongezeka kwa mujibu wa waandaaji kutoka wakimbiaji 750 wakati za kikianza hadi kufikia washiriki 11,000 kwa sasa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: