Saturday, 23 March 2019

MBUNGE ZAINAB KATIMBA NA MBARAZA UVCCM TAIFA ROSE MANUMBA WAONGOZA MJADALA WA BAJETIMbunge wa Viti Maalumu kutokea Kundi la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  Mhe. Zainab Katimba pamoja na Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana Taifa, Ndugu. Rose Robert Manumba ambaye pia ni Mratibu wa Vijana Taifa katika Asasi ya Kiraia YWCA Tanzania Jana walipata fursa yakukutana na kujadiliana na asasi mbali mbali za Vijana hapa Nchini kusikiliza mawazo na michango yao ya mambo ya kipaumbele kwa vijana  kwenye budget ya 2019/2020
Mhe. Mbunge Zainab Katimba Katika Mjadala Huo alivutiwa na Kijana Shupavu Mwenye Ulemavu wakutokusikia. Mhe Zainab alisema kuwawezesha watu wenye Ulemavu kutasaidia  kupunguza utegemezi wao kiuchumi. Mhe Zainab Katimba pia ni muasisi wa WEZESHA FOUNDATION taasis inayoshughulika na kuwezesha vijana na wanawake kwenye nyanja za uchumi na jamii.

Ndugu Rose Manumba aliongozana na Mhe Zainab Katiba Mbunge wa Vijana  baada ya Mbunge kupata Mwaliko kutoka Shirika la kijerumani FES ambalo limekuwa likitoa Mafunzo ya uongozi hapa nchini kwa muda mrefu na kusaidia kuinua vipaji vya vijana viongozi kwa muda mrefu.

Ndugu Rose Manumba aliwasilisha mada ya Vijana na Maendeleo ya Taifa letu. Rose alifafanua kuwa Jukumu la vijana ni  kuitunza na kuistawisha nchi yetu na sio kuiharibu. Tunao wajibu wa kutumia ujuzi tulionao kwaajili ya maendeleo ya Taifa letu. 

Alisisitza kuwa Vijana hatutakiwi kukaa vjiweni nakulalamika.Bado tuna nguvu kubwa na Afya. Huu ndio muda muafaka wakulitumikia Taifa Letu na Mh. Rais Magufuli anaimani kubwa Nasi vijana Ndiyo maana ameendelea kutuamini nakushirikisha Katika Serikali yake.

Imetolewa na Idara ya Waandaji wa mdahalo na Majadiliano Dar Es Salam  Tanzania

No comments:

Post a comment