NA HERI SHAABAN

MABALOZI wa Afya ya Uzazi wa Mpango MANISPAA ya Ilala imewataka Wananchi kutumia vituo vya kutolea huduma za afya na wataalam wa afya  kupata elimu ya afya ya uzazi  iliyo sahihi.

Tamko hilo limetolewa Dar es Salaam leo na   Mratibu wa Afya ya Uzazi wa Mpango Manispaa ya Ilala Edith Kijazi wakati wa  kikao cha Mabalozi wa afya ya Uzazi wa Mpango Manispaa hiyo, kikao kilichoandaliwa na manispaa ya Ilala idara ya Afya kwa kushirikiana na mdau, Shirika lisilo la kiserikali la JHPIEGO kwenye Mradi wa TCI Tupange pamoja. Lengo la Mradi likiwa ni   kupunguza vifo vya akina Mama na Watoto vinavyotokana na uzazi.

Kijazi aliongelea pia kuhusu huduma rafiki kwa vijana, alisema Wazazi wana kila sababu ya kutenga muda wa kuzungumza na watoto wao kuhusu mabadiliko katika ukuaji, changamoto watakazokutana nazo bila woga ili kuwasaidia watoto kuchukua maamuzi sahihi.mratibu alisema, " Mabalozi wa afya ya uzazi Manispaa ya Ilala tunawaomba mkazungumze na jamii watenge mda wa kukaa chini kuzungumza na watoto wao kuhusu afya ya uzazi kwani vijana wanakumbana na changamoto nyingi za kiafya ikiwemo mihemko ya kimwili, hivyo tusipowasaidia kuwapa elimu sahihi mapema ni rahisi kuharibikiwa "alisema Kijazi

Kijazi alisema jinsi Mtoto wako anavyokuwa una kila sababu ya kumueleza zuri na baya ili akikutana nalo aweze kuchukua maamuzi sahihi.

Kwa upande wake Katibu wa Wenyeviti wa serikali za mitaa Manispaa Ilala Mariam Machicha alisema Manispaa Ilala iandae Kauli Mbiu ya Afya ya Uzazi  itakayotumika kila wakati kwa ajili ya kufikisha ujumbe.

Machicha alisema kauli mbiu hiyo itawakumbusha kukemea wazazi ili vizazi vya sasa na vijavyo visimomonyoke kimaadili.

Naye Kaimu Mratibu wa Ufatiliaji na Tathimini idara ya afya Manispaa Ilala Anence Kamasho alisema manispaa inaendelea kutoa huduma rafiki kwa vijana kwa kushirikiana na wadau, ambapo kwa kipindi cha Jan- March 2019  walimu 100 na watoa huduma 30 wameweza kupatiwa mafunzo ya huduma rafiki ya afya ya uzazi kwa vijana.

 Aidha mijadala 10 ya vijana yaliyohusu afya ya uzazi yameweza kufanyika na  huduma ya mkoba pia imefanyika katika vyuo/shule 10 za binafsi na serikali zilizoko Manispaa ya Ilala.

Kuhusu Huduma ya Uzazi wa.  Mpango,
Balozi wa Uzazi wa Mpango Everline Mwakatuma aliomba Manispaa Ilala katika matukio matatu ,siku ya Wanawake Dunia, Siku ya Mtoto wa Afrika na siku ya MAMA ambayo yanafanyika kwa kila mwaka Elimu ya Uzazi wa Mpango epelekwe kwa ajili ya utoaji elimu kwa JAMII.

 Mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: