Thursday, 21 March 2019

Maalim Seif, Zitto Kabwe Watua Zanzibar na Kupokelewa na Mamia ya Wafuasi wa ACT- Wazalendo

Kiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe akiambatana na Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na viongozi na wanachama wengine wamewasili katika ofisi za chama hicho zilizopo Vuga, Mjini Unguja leo Machi 21, 2019 

Zitto amewasili katika ofisi mpya za ACT- Wazalendo zilizopo Vuga, Unguja ambazo awali zilikuwa makao makuu ya Chama cha Wananchi (CUF) visiwani humo.

Baada ya kuwasili katika ofisi hizo , Maalim Seif alimpokea Zitto huku mamia ya wana ACT- Wazalendo wakimpokea kwa nyimbo mbalimbali.

Zitto na Maalim walivalishwa mataji kisha wakaenda kukaa eneo maalum lililoandaliwa.

Alipopewa fursa ya kusalimia, Zitto amesema, “Nina furaha sana leo, nataka kuwahakikishia tumeshashusha tanga, tumeshapandisha tanga, safari inaendelea.

No comments:

Post a comment