Thursday, 21 March 2019

BIDHAA ZA MAGENDO YAKIWEMO MAGARI MATATU YANASWA MPAKANI WA TANZANIA NA ZAMBIA


Jeshi la polisi mkoani songwe limefanya msako mjini tunduma katika wilaya ya momba mkoani songwe na kufanikiwa kukamata bidhaa za magendo vikiwemo vinywaji ambavyo vilipigwa marufuku kuingia nchini na kutumika vyenye thamani ya shillingi million 745000 ambapo katika msako huo pia wamekamata magari matatu aina ya Noah.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa songwe GEORGE KYANDO amesema kuwa magari hayo yamekamatwa baada ya kuvushwa nchini zambia na kurejeshwa tanzania kwa njia ambazo sio halali...

Aidha katika tukio hilo watu sita wanashikiliwa katika katika kituo cha polisi Tunduma kwa mahojiano zaidi na bidhaa zote zilizokamatwa pamoja na magari hayo matatu .

Kamanda wa KYANDO ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kufichua watu ambao wanaisababishia hasara serikali kwa kupitisha bidhaa kwa njia ya magendo.No comments:

Post a comment