Tuesday, 19 March 2019

Askari mbaroni kwa kupiga dereva na abiria


Askari wawili wa Kikosi cha Usalama Barabarani wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa makosa ya kuwashambulia kwa matusi na kipigo, dereva na abiria wake.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni amesema baada ya kuona video hiyo aliagiza askari hao wakamatwe, na sasa wanasubiri kupelekwa mahakamani.

Alisema hao wapo kituo cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam wakisubiri kuchululiwa hatua na kuwataka wananchi wote pindi
wanapoona kuna vitendo ambavyo wanafanyiwa vilivyo kinyume cha sheria zetu wasisite kutoa taarifa kwetu.

Alisisitiza kuwa ikitokea uongozi wa askari unatetea au kutochukua hatua muafaka, mlalamikaji apande uongozi wa juu hata kwa Waziri na Naibu wake ili hatua zichukuliwe.

No comments:

Post a comment