Mbunge wa Korogwe vijijini ndugu Timotheo Mnzava leo tarehe 21/11/2018
amekutana na kufanya mazungumzo na mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya
Korogwe Bw. Kwame Daftari pamoja na wakuu wa idara.

Kikao hiko kifupi kilikuwa kimelenga zoezi la utambulisho baina ya mbunge na
watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Korogwe ikiwa ni katika kuunganisha
nguvu ya pamoja katika kuleta maendeleo endelevu kwa jimbo la Korogwe vijijini
na wilaya kwa ujumla.

Kikao hiko pia kilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Korogwe vijijini
ndugu Charles Mweta.

“Nimekuja kukutana nanyi nikiwa na lengo kuu la mimi kuwafahamu ila nanyi
mnifahamu, kwapamoja tuunganishe nguvu katika kuwatumikia wanakorogwe,
tupunguze kuzungumza sana na tuongeze uwezo wa kiutendaji ili tuendane na kasi
ya rais Mh. John Pombe Magufuli ya kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025,”
alisema Mh. Mnzava.

Aidha Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Korogwe, Bw. Daftari kwa niaba
ya wakuu wa idara ameahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa mbunge ili kufikia
lengo la kuleta matokeo chanya ambayo yataleta maisha bora kwa wananchi wa
Korogwe.

Imetolewa na,
Ofisi ya Mbunge, Korogwe Vijijini.
21/11/2018
Share To:

msumbanews

Post A Comment: