Saturday, 3 November 2018

Emmy Lema : Nitafanya Uzinduzi wa NguvuMWIMBAJI wa nyimbo za Injili, Emmy Lema amesema anatarajia kufanya uzinduzi mkubwa wa albamu yake inayokwenda kwa jina la Utukufu Hadi Utukufu  Uzinduzi huo utafanyika Novemba 11, mwaka huu na kupambwa na waimbaji wakubwa Injili akiwemo Mary Jane,John Shabani kutoka Dar es salaam pamoja na  Elizabeth Ngaiza kutoka Dar es salaam.

Akiuzungumzia uzinduzi huo utakaofanyika ndani ya Ukumbi wa Kuringe Garden Moshi Mjini,  Emmy alisema siku hiyo ambayo ni Jumapili, itakuwa ya kumsifu Mungu na kupokea miujiza kupitia sifa. “Niwakaribishe watu wote, hakutakuwa na kiingilio, waje washuhudie uzinduzi wa albam yangu ya Utukufu  Hadi Utukufu  na pia wataweza kuwasikia na kuwaona wanamuziki wenzangu wa muziki wa Injili,” alisema Emmy.

Emmy alisema mbali na waimbaji hao, waimbaji wengine watakaoupamba uzinduzi wake ni pamoja na Tumainisia Shao, Catherine Israel kutoka Dar es salaam pamoja na Lembo Juniour kutoka Dar es salaam

No comments:

Post a comment