Saturday, 3 November 2018

BreakingNews: Gari la CAG laua watu saba Dodoma

Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma Giles Muroto, amethibitisha kutokea vifo vya watu 7 katika ajali iliyohusisha magari mawili ya serikali ikiwemo, STL 6250 Toyota Land Cruiser kutoka ofisi ya CAG, baada ya kugongana uso kwa uso na gari yenye nambari SU 41173.

Kwa mujibu kwa kamanda Muroto katika ajali hiyo ambayo imetokea usiku wa kuamkia leo, pia watu watatu wamejeruhiwa kwenye ajali hiyo na wamelazwa katika hospitali za jirani zilizopo kwenye mkoa huo Dodoma kwa ajili ya huduma ya kwanza na miili ya marehemu kwa ajili ya kuhifadhiwa.

“Hii ajali inahusisha magari mawili ikiwemo Toyota Land Cruiser mali ya ofisi ya CAG iliyokuwa na jumla ya watu 7 yaligongana uso kwa uso na SU 41173, Toyota Land Cruiser mnali ya NSSF ambayo ilikuwa na watu 3, na kupelekea vifo vya watu 7 ajali ilitokea usiku wa kuamkia leo na jeshi la polisi linaendelea kuchunguza kufahamu chanzo kiundani ”, amesema Kamanda Mroto.

“Wito wangu kwa madereva ni hatari sana kusafiri usiku, lakini pia tumepoteza vijana wa serikali na wamesomeshwa na serikali, wito wetu magari yasafiri muda unaohitajika badala ya kusafiri usiku, na tutaanza kuwa wakali zaidi sababu wengine wanasafiri usiku, ili kukwepa tochi zetu”, amesema Kamanda Muroto

No comments:

Post a comment