Monday, 20 August 2018

Mgombea Ubunge wa CCM apita bila kupingwa Korogwe


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Timotheo Mnzava amepita bila kupingwa kwenye kinyang'anyiro hiki baada ya wagombea wenzake kutoka vyama vya upinzani kushindwa kurejesha fomu.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Korogwe ambaye ndiye msimamizi wa jimbo hilo, Dk George Nyaronga amethibitisha mgombea huyo wa CCM kupita bila kupingwa kutokana na kushindwa huko kurejesha fomu kwa muda uliopangwa kwa wagombea wa CUF, Chadema na ACT Wazalendo.

Jimbo la Korogwe Vijijini linafanya uchaguzi huo mdogo kumpata muakilishi wao kufuatia kifo cha aliyekua mbunge wao Stephen Ngonyani maarufu Majimarefu ambaye alifariki Dunia.

No comments:

Post a comment