Monday, 20 August 2018

DC JERRY MURO AAHIDI KUSIMAMIA UBORA WA ELIMU ARUMERU, AMSHUKURU RAIS KWA KUTOA PIKIPIKI KWA WARATIBU WA ELIMU


Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh.Jerry Muro akiwa na baadhi ya piki piki alizowakabidhi Waratibu wa elimu katika halmashauri ya wilaya ya Meru.


MKUU wa Wilaya Arumeru mkoani Arusha Jerry Muro amemshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa uamuzi wake wa kuendelea kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa vitendea kazi kwa lengo la kuboresha sekta hiyo huku akiahidi kusimamia ubora wa elimu.

Muro amesema hayo wakati anakabidhi Pikipiki mpya 18 kwa waratibu wa elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambazo zimetolewa na Rais kupitia Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, ikiwa sehemu ya mkakati wa Serikali ya Awamu ya Tano Chini ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli ya kufuatilia Ubora wa Elimu Nchini.

"Tunashukuru kwa vitendea kazi hivi ambavyo tumepewa na Rais kupitia Waziri wa Elimu.Tunaamini vitendea kazi hivi vitatumika kwa lengo ambalo limekusudiwa.

" Tutahakikisha tunainua kiwango cha ufaulu katika Halmashauri yetu ya Arumeru pamoja na kuinua kiwango cha elimu.Lengo ni kuhakikisha mtoto wa maskini anapata elimu iliyo bora,"amesema.

Amefafanua kuwa kupatikana kwa pikipiki hizo na kisha kuzigawa kwa waratibu wa elimu wilayani huo kunatoa nafasi ya wao kutimizamajukumu yao ya kufuatilia ubora wa elimu katika shule za Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru.

No comments:

Post a comment