Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Ustawi wa jamii, Jinsia na Walemavu Mhe Ummy Mwalimu alivyo tembelea mradi wa ujenzi wa Wodi ya Mama na Watoto utakao gharimu fedha taslimu za kitanzani shilling Bi tano 5,000,000,000 katika hospital ya Mkoa wa Mwanza.

Mhe Ummy amesema miongoni mwa vipaumbele vya serikali ni kutokomeza vifo vinavyotokana na magonjwa yanayo tokana na Uzazi pamoja na vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano. Kwa dhamira hiyo wameamua kujenga wodi ya Mama na Mtoto itakayo toa huduma za kibingwa ili kusogeza huduma karibu na jamii sanjari na kuondoa msongamano katika hospital ya rufani ya kikanda Bugando.

Mhe Ummy Mwalimu aliambana na mwenyeji wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ndg Mary Tesha, Mganga mkuu wa Mkoa, Mbunge Jimbo la Nyamangana Mhe Stanslaus Mabula, Mwenyekiti wa Bodi ya hospital Mhe Christopher Gachuma pamoja na viongozi wengine wa wizara na serikali.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Share To:

msumbanews

Post A Comment: