Sunday, 22 July 2018

Serikali kusimama na wajasiliamali kuelekea uchumi wa viwanda


Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amesema Serikali itaendelea kuwaunga mkono wanawake katika shughuli zao za ujasilimali ili waweze kuanzisha viwanda vidogo vidogo na kujiongezea kipato.

Mjema Ameyasema hayo leo julai 21 kwenye Kongamano la Changamka Mwanamke lililo fanyika  Ilala jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa wanawake wanao uwezo mkubwa  wa kubuni biashara lakini wameshindwa  katika mitaji.

"Nimepita hapa nimekuwa Juice ya viazi lishe, sijawahi kunywa nimeona ni ubunifu wa hali ya juu naninzuri  mama huyu alichoshindwa ni kuboresha vifungashio ili kuboresha biashara yake hilo nimeliona tutasaidiana" Amesema.

Amesema baadhi ya mambo ambayo yamekuwa ni changamoto ni pamoja na  nembo ya Biashara, TFDA na mashine za EFD ambazo kwa sasa zina uzwa beighali.

"Hawa wote tunafanya nao kazi katika serikali hii ntawaita tutazungumza nao waweze kuona namna ya kutusaidia ili tuendelee biashara zetu nami nitawasaidia " Amesema.

Aidha amewasisitiza wanawake hao kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na Manispaa ya Ilala ambayo kwaajili ya akina mama.

" Kuna mifuko 19 ya kuwezesha wananchi kiuchumi serikalini mnaweza pia kuitumia hii mifuko kufanya biashara na kuanzisha viwanda vidogo vidogo"amesema.

Kwaupande wake Mkurugenzi mwanzilishi wa Changamka Mwanamke  Maria Lukas amemwomba mkuu wa Wilaya Sophia Mjema  kuwasaidia wanawake hao kupata mitaji na kuwawezesha kupata mikopo ili waendeleze biashara zao.

Na kuahidi kuwa  taasisi hiyo itaendelea kufanya kazi za kujitolea katika jamii na kwamba wanampango wa kuanzisha kilimo cha pilipili na kuimarisha umoja wao

No comments:

Post a comment