Wednesday, 25 July 2018

RC Mnyeti akanusha kuwepo kwa wizi wa madini ya Tanzanite


Na John Walter manyara
Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexender Mnyeti amewataka wananchi kusikiliza taarifa zinazotolewa na vyombo vya serikali na sio kusikiliza taarifa mitaani kwani hizo zinapotosha .

Kauli hiyo ameitoa baada ya kuzuka kwa taarifa kuwa madini ya Tanzanite yanaibiwa licha ya kuwepo kwa ukuta ulijengwa kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mererani katika wilaya ya Simajiro.

Ameeleza kuwa ulinzi umeimarishwa katika kila kona ya eneo la ukuta wa Tanzanite pamoja na Kamera huku kila anaetoka akikaguliwa mlangoni hivyo hakuna uwizi wowote unaofanyika.

Mnyeti ameeleza kuwa 'Ni kweli miaka ya nyuma wizi wa madini ya Tanzanite ulikuwa ukifanyika lakini kwa sasa kutokana na uimara wa jeshi la polisi mkoa wa Manyara hakuna mwanya wa kufanyika wizi hu,".

AidhaMnyeti amesesma kuwa wanaosema madini yanatoroshwa kama wanao ushaihidi wautoe ili watu hao wakamatwe.

No comments:

Post a comment