Mkuu wa wilaya ya Monduli Mh.Idd Hassan Kimanta jana alitembelea wahanga wa janga la moto huko katika kata Engaruka kijiji cha Irerendeni. 

Mkuu wa wilaya akifatana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama na Mh.Julias Kalanga Mbunge wa Jimbo la Monduli walijionea adha iliyokumba wafanyabishara hao kwa kuunguliwa na vibanda vyao vya maduka  Moto huo ulionza mnamo tarehe 17.07.2018 saa saba usiku na kudumu kwa saa tano umeleta athari kubwa na kifo kwa mfanyabiashara mmoja ajulikanae kwa jina la Siriel massawe mauti yalimkuta mara baada kuzidiwa na moto mkubwa ndani.

Maduka saba yaliteketea Dc Kimanta akizungumza na wahanga hao aliwapa pole na aliwataka kuwa watulivu kwanza huku vyombo vya ulinzi vikifanya uchunguzi.

Pia kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Monduli imeahidi kutoa mkono wa pole Tsh.200.000/= kwa kila mfanyabiasharana kuwalipia madeni ya Mikopo yao waliokopa Kwenye Taasisi za Kifedha Mara baada kuhakiki mikopo yao. 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: