Tuesday, 17 July 2018

DC HOMERA APOKEA PIKIPIKI 39 KWAAJILI YA WARATIBU ELIMU KATA


Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera amepokea jumla ya Pikipiki 39 kutoka kwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Wizara yake ya TAMISEMI.

akiongea wakati wa kupokea Pikipiki hizo DC Homera amemshukuru Mh Rais kwa kuwa na nia njema na dhamira ya dhati ya kuinua kiwango cha elimu tanzania na Wilaya ya Tunduru kwa Ujumla.

Amesema dhamira ya dhati aliyokua nayo Mh.Rais sio tu ya kugawa Pikipiki peke yake bali pia kwa kuboresha Maslahi ya Watendaji katika Sekta Elimu wakiwemo Waratibu wa Elimu na Wakaguzi kwa Ujumla.

Ameongeza kuwa wilaya ya Tunduru imeweza kushika nafasi ya pili kwa Ufaulu kwa kupata jumla ya asilimia 86 katika Mtihani wa moko wa Mkoa wa Ruvuma  jambo ambalo halikuwepo kwa muda mrefu Mkoani humo na hivyo kuwataka Watendaji wote kuunga Mkono jitihada za Mh.Rais Magufuli kwa kufanya kazi kwa Bidii.

Aidha Homera ametoa mwito kwa Watendaji wote watakao tumia Pikipiki hizo kuzitunza na kuhakikisha wanazitumia katika Matumizi yaliyokusudiwa na sio kuzifanyia Shughuli nyingine zikiwemo kubeba Mkaa. 

Kwa upande wake Afisa kutoka Wizara ya TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya Vifaa na Usambazaji Salum Mkuya,amewataka watendaji hao kufanya kazi ipasavyo kwa kuhakikisha wanafatilia kwa ukaribu katika shule zote za Msingi na Sekondari namna ya ufundishaji wa walimu darasani kwa kufuata taratibu zote na Mtalaa uliopo.  

No comments:

Post a Comment